Pata taarifa kuu
TERRY-USAJILI-ULAYA

Terry agusia kuachana na klabu yake ya Chelsea mwishoni mwa msimu, huku usajili wa dirisha dogo leo ukifikia tamati

Nahodha wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, John Terry ameeleza nia yake ya kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu, baada ya uongozi kushindwa kumpa mkataba mwingine.

Beki wa kati wa Chelsea, John Terry ambaye ametangaza ataachana na klabu yake mwishoni mwa msimu
Beki wa kati wa Chelsea, John Terry ambaye ametangaza ataachana na klabu yake mwishoni mwa msimu
Matangazo ya kibiashara

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 35 hivi sasa alijiunga na the Blues akiwa na umri wa miaka 14 na kucheza mechi 696 akiwa na Chelsea, ambapo ameshinda mataji manne ya ligi kuu, mataji matano ya kombe la FA pamoja na klabu bingwa ulaya.

Terry anasema kuwa yeye binafsi angependa kusalia kwenye klabu hiyo, lakini inavyoonekana ni kuwa klabu hiyo inauelekeo mwingine ambao hata hivyo hakuutaja.

Sababu kubwa ya John Terry kutangaza mapema kuwa ataachana na timu yake hiyo mwishoni mwa msimu, kumetokana na uongozi wa Chelsea kushindwa mpaka sasa kumsainisha mkataba mwingine wa kuitumikia timu hiyo.

John Terry celebrates with team mates after scoring the second goal for Chelsea
John Terry celebrates with team mates after scoring the second goal for Chelsea Reuters/Carl Recine

Hata hivyo, msemaji wa klabu ya Chelsea, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Terry kuongezewa mkataba.

Terry anasema baada ya kuachana na Chelsea anatarajia kuendelea kucheza soka lakini hatamani kusalia ncini Uingereza na badala yake analenga kucheza nje ya Uingereza.

Wachezaji kadhaa wakongwe wameandika kwenye mitandao yao ya kijamii huku wengine wakisikitishwa na uongozi wa Chelsea kushindwa kumpa mkataba mwingine, huku wachache wakiunga mkono uamuzi wake huo na wengine wakitaka wasalia.

Kuhusu masuala ya usajili:

Kuhusu masuala ya usajili wa dirisha dogo barani Ulaya, tayari vilabu kadhaa ikiwa leo ndio siku ya mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, vimeshakamilisha kupata saini ya baadhi ya wachezaji.

Seydou Doumbia
Seydou Doumbia REUTERS/Darren Staples

Miongoni mwa usajili uliokamilika ni pamoja na ule wa mshambuliaji Seydou Doumbia anaejiunga kwa mkopo na klabu ya Newcastle akitokea Roma, Jonjo Shelvey akitokea Swansea anajiunga na Newcastle kwa dau la paundi za Uingereza 12.

Wengine waliokamilisha usajili ni pamoja na Andros Townsend aliyejiunga na klabu ya Newcastle akitokea Tottenham kwa dau la pandi milioni 12, wengine ni Emmanuel Emenike anayejiunga na klabu ya West Ham akitokea Fenerbache ya Uturuki kwa mkopo, Matt Miazga amejiunga na Chelsea akitokea klabu ya New York Red Bulls kwa dau ambalo halijawekwa wazi.

Wengine ni Alexandre Pato aliyejiunga na klabu ya Chelsea akitokea timu ya Corinthians kwa mkopo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.