Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Makocha wa vlabu vya Ulaya wakumbwa na kizungumkuti

Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger anasema amesikishwa na uvumi kuwa kocha wa Manchester United Louis van Gaal huenda akafutwa kazi baada ya kushindwa kupata ushindi katika michuano sita iliyopita.

Arsène Wenger, meneja wa Arsenal.
Arsène Wenger, meneja wa Arsenal. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na uvumi kuwa aliyekuwa kocha wa Chelsea aliyefutwa kazi wiki iliyopita Jose Mourhino huenda akapewa kibarua cha kuifunza Manchester United.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akifuatilia moja ya mechi ya timu yake
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akifuatilia moja ya mechi ya timu yake GettyImage

Wenger amesema kuwa sio jambo jema kwa yeyote kufutwa kazi kwa sababu ni jambo la huzuni sana.

Baada ya kufungwa na klabu ya Norwich mabao 2 kwa 1 mwishoni mwa juma lililopita, Vaan Gaal amesema ana wasiwasi kuhusu nafasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.