Pata taarifa kuu
ZAMBIA-MSUMBIJI-SOKA

Zambia na Msumbiji zapiga hatua

Zambia na Msumbiji zimeanza vizuri safari yao ya kufika katika hatua ya makundi kufuzu katika fainali ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Mchezaji wa Zambia Nathan Sinkala (kulia) akikabiliwa na mchezaji wa Congo Spencer Sautu.
Mchezaji wa Zambia Nathan Sinkala (kulia) akikabiliwa na mchezaji wa Congo Spencer Sautu. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Zambia ikicheza jijini Khartoum siku ya Jumatano, iliwafunga wenyeji wao Sudan bao 1 kwa 0 na Msumbuji ikicheza nyumbani jijini Maputo iliifunga Gabon pia kwa bao 1 kwa 0.

Michuano hiyo inaendelea siku ya Alhamisi jioni katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Jijini Lome, Togo ni wenyeji wa Uganda kutoka Afrika Mashariki na mchuano mwingine unachezwa ni kati ya Burundi ambao wanawakaribisha jirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Bujumbura.

Michuano ya marudiano itachezwa wiki ijayo na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi ili kuendelea na michuano ya kutafuta mataifa matano yatakayowakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo ya dunia.

Ratiba nyingine siku ya Alhamisi:

Namibia vs Guinea
Morocco vs Equatorial Guinea
Benin vs Burkina Faso

Siku ya Ijumaa Ijumaa Novemba 13 2015

Kenya vs Cape Verde
Madagascar vs Senegal
Liberia vs Ivory Coast
Comoros vs Ghana
Mauritania vs Tunisia
Niger vs Cameroon
Libya vs Rwanda
Angola vs Afrika Kusini

Siku ya Jumamosi Novemba 14 2015

Tanzania vs Algeria
Ethiopia vs Congo
Chad vs Misri
Bostwana vs Mali

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.