rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

New Zealand

Imechapishwa • Imehaririwa

Sherehe nchini New Zealand baada ya kunyakua kombe la dunia

media
New Zealand mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2015

Sherehe zinaendelea mjini Wellington na Christchurch baada ya New Zealand kushinda taji la dunia katika mchezo wa raga kwa mara nyingine tena.


New Zealand wanaofahamika kwa jina maarufu kama All Black, pia walishinda taji hili mwaka 2011 na mwishoni mwa juma lililopita walionesha kuwa wao ndio mabingwa wa mchezo huu duniani kwa kuwafunga Australia kwa alama 34 kwa 17 katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa Twickenham jijini London na kuhudhuriwa na mashabiki zaidi ya elfu 80.

Wachezaji wa Newzealand wakicheza Haka kabla ya mchezo

Nicolas Sanchez kutoka Argetina aliyeifungia timu yake alama 97 ndiye aliyeibuka mfungaji bora huku Julian Savea kutoka Australia naye akaibuka mchezaji aliyefunga try nyingi katika mashindano haya ambazo zilikuwa nane.

Wawakilishi wa Afrika katika michuano hiyo, Afrika Kusini walimaliza katika nafasi ya tatu na kujinyakulia medali ya shaba baada ya kuwashinda Argentina alama 24 kwa 13.

Kikosi cha New Zealand kikijiandaa kabla ya mchezo wa fainali

Kombe la dunia la mwaka 2019 litafanyika nchini Japan.