Pata taarifa kuu
ASTON VILLA-SOKA

Remi Garde kocha mpya wa Aston Villa

Siku ya Jumatatu klabu ya Aston Villa inatazamia kusaini mkataba na meneja wa zamani wa klabu ya Ufaransa, Lyon,  baada ya kumfuta kazi kocha wake Tim Sherwood.

Jimmy Briand akiwa pamoja na kocha wake Rémi Garde.
Jimmy Briand akiwa pamoja na kocha wake Rémi Garde. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Rémi Garde atasaini mkataba wa miaka mitatu na nusu. Na atakuwepo katika mchuano wa Jumatatu wiki hii dhidi ya Tottenham ugenini. Raia huyo wa Ufaransa ataketi katika eneo wanakoketi mashabiki.

Rémi Garde, mwenye umri wa miaka 49 anachukua klabu Aston Villa ikiwa inashika mkia katika Ligi ya Premia. Klabu hiyo ilipata alama nne pekee kwa jumla mechi 10 iliyocheza.

Rémi Garde alisaidia Lyon kumaliza nambari nne, tatu na tano katika misimu mitatu aliyokuwa nao kuanzia 2011 kabla ya kuwaacha 2014 kutokana na sababu za “kibinafsi na kifamilia”.

Kocha wa Bastia Reginald Ray atakayekuwa msaidizi wa Garde. Wawili hao watasimamia mechi yao ya kwanza nyumbani dhidi ya Manchester City Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.