rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Yanga SC Simba SC Azam FC

Imechapishwa • Imehaririwa

Yanga yapata ushindi wa pili mfululizo

media
Mji wa Dar es Salaam ambako mechi mbalimbali zinapigwa msimu huu. Getty Images/Ariadne Van Zandbergen

Ligi Kuu ya Tanzania bara iliendelea siku ya Jumatano huku mabingwa watetezi Yanga FC wakipata ushindi wa pili mfululizo.


Wanajwagani hao wakicheza mchuano wake wa pili katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam waliwashinda Tanzania Prisons mabao 3 kwa 0.

Mabingwa wa zamani nao waliendeleza ushindi wao baada ya kuishinda JKT Mgambo mabao 2 kwa 0.

Maji Maji ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City nao wakapata ushindi mkubwa wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Ruvu Stars.

Matoke mengine, Azam FC 2 Stand United 0, Mtibwa Sugar 2 Toto Africans 1, Ndanda 1 Coastal Union 0 na Mwadui 2 African Sports 0.

Michuano hiyo inaendelea siku ya Jumamosi:-

JKT Mgambo-Maji Maji
Stand United-African Sports
Tanzania Prisons-Mbeya City
Young Africans-Ruvu Stars

Jumapili:

Mwadui- Azam
Mtibwa Sugar- Ndanda
Simba- Kagera Sugar
Costal Union-Toto Africans.