Pata taarifa kuu
WIMBLEDON-TENESI

Djokovic, Serena na Sharapova kusaka nafasi ya kucheza 16 bora michuano ya Wimbledon

Michuano ya tenesi ya Wimbledon imeendelea kushika kasi huku ikiingia siku yake ya tano hii leo, ambapo mchezaji nambari moja kwa upande wa wanaume Novak Djokovic akitarajiwa kutupa karata yake kufuzu hatua ya kumi na sita bora, sambamba na mchezaji bora kwa upande wa wanawake, Serena Williams na Maria Sharapova.

Mchezaji Rafael Nadal ambaye juma hili ameondoshwa kwenye michuano ya Wimbledon
Mchezaji Rafael Nadal ambaye juma hili ameondoshwa kwenye michuano ya Wimbledon REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hawa watatupa karata zao kukabiliana na wachezaji ambao hawana majina, katika mechi ambazo zinatarajiwa kuwa na upinzani, hasa ukizingatia kuwa bingwa mara 14 wa michuano ya kimataifa Muhispania Rafael Nadal akitolewa kwenye muchuano ya mwaka huu.

Novak Djokovic, Serena Williams and Maria Sharapova target Wimbledon last-16 places on Friday, hoping to avoid the underdog trap that claimed two-time winner Rafael Nadal.

Katika mechi zilizochezwa hapo jana, mchezaji James Ward wa Uingereza alimfunga Jirí Veselý wa Jamhuri ya Czech kwa seti 6-2, 7-6, 3-6 na 6-3, huku mchezaji Vasek Pospisil wa Canada akimfunga Fabio Fognini wa Italia kwa seti 6-3, 6-4, 1-6 na 6-3.

Viktor Troicki wa Serbia yeye alitinga hatua inayofuata kwa kumfunga Aljaz Bedene wa Uingereza kwa seti 6-4, 3-6, 6-2 na 6-4, huku Mjerumani Dustin Brown akimduwaza mchezaji nambari 10 kwa ubora Muhispania Rafael Nadal kwa seti 7-5, 3-6, 6-4 na 6-4, huku Jo-Wilfried Tsonga wa Ufaransa akimfunga Albert Ramos wa Uhispania kwa seti 6-3, 6-4 na 6-4.

Kwenye mechi nyingine mchezaji Andreas Seppi wa Italia alimfunga Borna Coric wa Croatia kwa seti 4-6, 6-4, 6-7, 6-1 na 6-1, huku Andy Murray wa Uingereza akimfunga Robin Haase wa Uholanzi kwa seti 6-1, 6-1, 6-4, wakati Tomas Berdych wa Jamhuri ya Czech akimfunga Nicolas Mahut wa Ufaransa kwa seti 6-1, 6-4, 6-4, huku Roger Federer wa Uswisi anayeshikilia nafasi ya pili kwa ubora akimfunga Sam Querrey wa Marekani kwa seti 6-4, 6-2 na 6-2.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji Caroline Wozniacki wa denmark alimfunga Denisa Allertová wa Jamhuri ya Czech kwa seti 6-1, 7-6, huku Angelique Kerber wa Ujerumani akimfunga Anastasia Pavlyuchenkova wa Urusi kwa seti 7-5, 6-2, wakati Kristýna Plísková wa jamhuri ya Czech akimfunga Svetlana Kuznetsova wa Urusi kwa seti 3-6, 6-3, 6-4.

Mechi nyingine iliwakutanisha Magdaléna Rybáriková ambaye alimfunga Ekaterina Makarova wa Urusi kwa seti 6-2, 7-5, huku Agnieszka Radwanska wa Poland akimfunga Ajla Tomljanovic wa Croatia kwa seti 6-0, 6-2.

Hii leo kutakuwa na mechi nyingine za kusaka nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora ambapo kwa upande wa wanawake, mchezaji Serena Williams atacheza na Heather Watson, huku Aleksandra Krunic atacheza na Venus Williams.

Mechi nyingine kwa upande wa wanawake, Kristina Mladenovic atacheza na Victoria Azarenka wakati Maria Sharapova atacheza na Irina Camelia Begu.

Kwa upande wa wanaume, mchezaji Novak Djokovic atacheza na Bernard tomic, huku Grigor Dimitrov atacheza na Richard Gasquet, wakati Stan Wawrinka atacheza na Fernando Verdasco.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.