Pata taarifa kuu
COPA AMERICA-ARGENTINA

Argentina kucheza fainali na wenyeji Chile kwenye michuano ya Copa America

Timu ya taifa ya Argentina imejiweka kwenye mazungira mazuri zaidi ya kuweza kutwaa taji la kombe la Bara Amerika Kusini "Copa America" kwa mara ya kwanza toka ilipofanya hivyo mwaka 1993 baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 6-1 usiku wa kuamkia leo dhidi ya Paraguay.

Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akiwania mpira na mchezaji wa Paraguay, Paulo da Silva.
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akiwania mpira na mchezaji wa Paraguay, Paulo da Silva. REUTERS/Mariana Bazo
Matangazo ya kibiashara

Mazingira haya yamekuja baada ya usiku wa kuamkia leo kufanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya timu ya taifa ya Paraguay ambapo sasa timu hiyo itacheza fainali na wenyeji wa michuano hii, timu ya taifa ya Chile.

Argentina ambao katika mchezo huo toka mwanzo ilionesha kuwa ilidhamiria kuibuka na ushindi, haikuchukua muda sana kupata bao lake la kwanza ambapo kufuatia mpira wa faulo ya Lionel Messi, mpira ulimkuta Marcos Rojo na kuipa bao la kuongoza timu yake katika dakika ya 15 ya mchezo.

Wachezaji wa Chile wakishangilia moja ya mabao waliyofungwa kwenye mechi za Copa America
Wachezaji wa Chile wakishangilia moja ya mabao waliyofungwa kwenye mechi za Copa America Reuters/Ivan Alvarado

Argentina baada ya kupata bao hilo ilianza kufanya mashambulizi mfululizo kwenye lango la wapinzani wao, ambapo katika dakika ya 27 mchezaji Javier Pastore aliiandikia timu yake bao la pili.

Hata hivyo Paraguay ilijibu mapigo na kufanikiwa kupata bao moja kupitia kwa Lucas Barrios aliyepiga shuti kali akiwa umbali wa mita 20 na kufanya matokeo hayo kuwa 2-1.

Katika dakika ya 47 ya mchezo, winga wa Argentina anayekipiga na klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Angel Di Maria, aliiandikia timu yake bao la tatu, kabla ya dakika ya 53 ya mchezi kuiandikia timu yake bao jingine na kufanya matokeo kuwa 4-1.

Mchezaji anayekipiga na klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Sergio Aguero aliiandikia timu yake bao la tano kayika dakika ya 80 kabla ya mshambuliaji Gonzalo Higuain kupachika bao la 6 na laushindi kwa timu hiyo akipokea pasi kutoka kwa Lionel Messi.

Licha ya kushindwa kupachika bao lolote kwenye mechi hiyo, mchezaji Lionel Messi alikuwa mwiba kwa timu ya Paraguay ambayo wachezaji wake walionekana kupata shida kumlinda mchezaji huyo aliyetumia vyema kipaji chake na kusababisha mabao manne kati ya sita yaliyofungwa na timu yake.

Huu ulikuwa ushindi wa kuvutia kwa kikosi cha kocha Gerardo Martino ambaye kikosi chake sasa kimekata rasmi tiketi ya kucheza fainali na wenyeji Chile katika uwanja wa Santiago July 4 mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.