Pata taarifa kuu
GHANA-ALGERIA-SOKA-AFCON 2015

Ghana yaiburuza Algeria

Black Stars, timu ya taifa ya Ghana baada ya kufungwa na Senegal katika mechi yake ya kwanza, imejipatia ushindi Ijumaa Januari 23 kwa kukuifunga Algeria katika dakika za mwisho bao 1-0. Kwa sasa Ghana inaendelea na michuano katika hatua ya robo fainali.

Mchezaji wa Ghana, Christian Atsu (kushoto) akimdondosha mchezaji wa Algeria, Faouzi Ghoulam (kulia) wakati wa mechi ya siku ya pili ya Kundi C ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 Ijumaa, Januari 23.
Mchezaji wa Ghana, Christian Atsu (kushoto) akimdondosha mchezaji wa Algeria, Faouzi Ghoulam (kulia) wakati wa mechi ya siku ya pili ya Kundi C ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 Ijumaa, Januari 23. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Algeria ambayo imekua imepewa nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo ilijikuta inaambulia patupu baada ya kuburuzwa na Ghana.

Mashabiki wa Algeria wamepigwa na butwaa kuona hadi dakika ya mwisho wanajikuta wamepoteza alama tatu.

“ Nitaifuata timu ya taifa ya Algeria popote pale itajielekeza, iwe ni eneo kunakoripotiwa Ebola au la”, amesema shabiki mmoja wa timu hiyo akitokea Mongomo kuhudhuria mechi kati ya Algeria na Ghana, lakini ameelezea masikitiko yake kuona Algeria imefungwa katika dakika za mwisho.

Katika mechi ya awali, Algeria iliibuka mshindi dhidi ya Afrika Kusini, lakini wengi waliona kuwa Algeria, wakati huo, ilipata ushindi kwa bahati.

Kocha wa Ghana, Avraham Grant, amesema walikua na matumani ya kushinda mchuano kati yake na Algeria", amesema Avraham Grant.

“ Tulikua na matumaini sana na Asamoah Gyan, ambae hali yake ya afya sio nzuri na hakua akifanya mazoezi. Lakini ni nahodha mkubwa na mchezaji kubwa. Fikiria kama angeweza kucheza mchezo wa kwanza, na kufanya jitihada hizo alizofanya katika mechi hii ya pili kwa zaidi ya dakika tisini wakati bado hali yake ya afya ni dhaifu”, ameongeza Avraham Grant.

 

Kundi C

Naf Timu M Al
1 Senegal 2 4
2 Ghana 2 3
3 Algeria 2 3
4 Afrika 2 1

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.