Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA / ULAYA

Ligi ya mabingwa: Real Madrid yaimenya Liverpool

Real Madrid imechuana na Liverpool Jumatano Oktoba 22 jioni katika siku ya tatu ya mzunguko wa makundi ya ligi ya Mabingwa. Wakati ambapo Juventus haikuafanya vizuri, huku Arsenal ikionesha muujiza ugenini.

Karim Benzema, aliye itoa pabaya Real Madrid, ambayo imekua na furaha baada ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Liverpool, Jumatano Oktoba 22mwaka 2014.
Karim Benzema, aliye itoa pabaya Real Madrid, ambayo imekua na furaha baada ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Liverpool, Jumatano Oktoba 22mwaka 2014. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jumanne usiku, vilabu vikuu vinavyoongoza katika michuano hiyo, ikiwa ni pamoja na PSG, ambayo iliibuka mshindi dhidi ya Nicosia kwa bao 1-0. Chelsea ikaishinda Maribor mabao 7-0. Nayo Bayern Munich iliimenya AS Roma mabao 7-1. Barcelona kwa upande wake iliifunga Ajax Amsterdam mabao 3-1.

Katika mchuano uliyochezwa Jumatano Oktoba 22 kati ya Real Madrid na Liverpool, Liverpool imeshindwa kufanya vizuri ikiwa nyumba, wakati ambapo mashabiki wa klabu hiyo waliamini watafanya vizuri wanapochezea nyumbani.

Mashabiki wa Real Madrid wameisifu klabu yao na kubaini kwamba walikua na imani kwamba watafanya vizuri wakiwa ugenini, kwani katika mchezo huo ilionekana dhahiri kwamba Real Madrid ilikua ikiipa Liverpool somo la soka, wamesema mashabiki wa Real Madrid.

Katika mchezo huo nyota wa Real Madrid, Karim Benzema aliifungia klabu yake mabao mawili (katika dakika ya 30 na 41). Katika dakika ya 70 ya mchezo, Ronaldo alipachika bao la tatu na kuandikisha mabao 70 ambayo ameingiza wavuni katika michuano ya ligi ya mabingwa.

Arsenal imeonesha muujiza katika za mwisho ilipokua ikicheza na Anderlecht ya Ubelgiji. Hadi dakika ya 85 klabu ya Anderlecht ilikua inaongoza bao 1-0 dhidi ya Arsenal. Katika dakika ya 89 mchezaji wa Arsenal Gibbs alisawazisha na baada ya dakika 2 ya bao hilo Podolski alichezesha wavu wa klabu ya Anderlecht.

Arsenal inachukua nafasi ya pili katika kundi D.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.