Pata taarifa kuu
AFRIKA-SOKA-MICHEZO

CAN 2015: Mali yashinda kwa kishindo

Baada ya kushindwa kufanya vizuri nchini Algeria, timu ya taifa ya Mali imeimenya Ethiopia Jumamosi Oktoba 11 mwaka 2014 kwa mabao 2 kwa nunge. Mali inashika nafasi ya pili katika kundi B, baada ya kushinda mechi mbili kati ya tatu ambazo imeshacheza.

Mali yapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia, lakini nahodha wake Seydou Keita aondolea nje ya uwanja baada ya kupata jeraha.
Mali yapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia, lakini nahodha wake Seydou Keita aondolea nje ya uwanja baada ya kupata jeraha. AFP PHOTO / BEN STANSALL
Matangazo ya kibiashara

Nyota wa timu ya taifa ya Mali, Seydou Keita, hakucheza dakika 90 za mchezo kutokana na jeraha alilopata katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Abdoulaye Diaby, mwenye umri wa miaka 23, akiwa ni mshambuliaji wa klabu ya Mouscron (Ubelgiji), ambaye ni kwa mara ya kwanza anashiriki michuano hiyo ametamba katika uwanja wa mpira wa mjini Addis Ababa. Mshambuliaji huyo wa klabu ya Mouscron , aliyenolewa Sedan hadi sasa ameingiza wavuni mabao saba tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Bao lakwanza la Mali limeingizwa katika dakika 33 ya mchezo, huku Sambou Yatabare akiingiza bao la pili katika dakika ya 66 kupitia pasi ya Abdoulaye Diaby

Kufuatia mabao hayo mawili kwa nunge dhidi ya Ethipia, Mali imejikuta ikiwa kwenye nafasi nzuri baada ya kushindwa kufanya vizuri nchini Algeria mwezi Septemba ambapo ilifungwa bao 1 kwa nunge. Iwapo Mali itaishinda Ethiopia kwa mara nyingine Oktoba 15, itakua imejikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika (CAN 2015).

Kundi B linapangwa ifuatavyo

 
                           Alama         Mabao      Dhidi             +/-                 Mechi
 

1. Algeria                 9                     5           1                +4                      3

2. Mali                      6                     4           1               +3                       3

3. Malawi                 3                     3            6               - 3                       3

4. Ethiopia               0                     3            7               - 4                       3
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.