Pata taarifa kuu
BRAZIL 2014

Brazil, Ujerumani, Uholanzi na Argentina zafuzu nusu fainali

Wenyeji Brazil pamoja na mataifa ya Ujerumani, Uholanzi na Argentina yamefuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya soka ya kombe la dunia inayoendelea nchini Brazil. 

Wachezaji wa Uholanzi wakisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali
Wachezaji wa Uholanzi wakisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali FIFA.COM
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa, Ujerumani iliyokuwa ya kwanza kufuzu katika hatua ya nusu fainali iliifunga Ufaransa bao 1 kwa 0 katika mchuano ulioonekana mgumu kati ya timu hizi mbili.

Mats Hummels ndiye aliyeipa ushindi Ujerumani kupitia bao hilo alilolifunga dakika 12 ya mchuano huo, ambao wachambuzi wa soka wanasema timu zote mbili zilikuwa zinacheza kwa kuogopana na pia nafasi nyingi za kutafuta mabao hazikuundwa kama ilivyokuwa katika hatua ya makundi.

Ujerumani ikimenyana na Ufaransa
Ujerumani ikimenyana na Ufaransa FIFA.COM

Wenyeji Brazil nao waliwashinda Colombia mabao 2 kwa 1 na kufuzu katika hatua muhimu ya nusu fainali na kuweka matumaini hai ya kunyakua taji hili kama wenyeji.

Mabao ya Brazil yalitiwa kimyani na Thiago Silva katika dakika ya 7 huku David Luiz akiongeza la pili na la ushindi katika dakika ya 68.

James Rodrigues aliwapa vijana wa Colombia bao la kusawazisha katika dakika ya 80 kupitia mkwaju wa Penalti.

Mchezaji wa Brazil David Luiz
Mchezaji wa Brazil David Luiz

Jumamosi usiku, Argentina walifuzu baada ya kuwashinda Ubelgiji bao 1 kwa 0, bao lililotiwa kimyani na Gonzalo Higuain.

Argentina inafika katika hatua hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990.

Mshambulizi matata Lionell Messi amefikia rekodi ya Diego Maradona ya kuichezea timu yake ya taifa mechi 91.

Wachezaji wa Argentina wakisherekea ushindi shidi ya Ubelgiji
Wachezaji wa Argentina wakisherekea ushindi shidi ya Ubelgiji FIFA.COM

Uholanzi ilikuwa timu ya mwisho kufuzu baada ya kushinda Costa Rica kwa mabao 4 kwa 3 kupitia mikwaju ya Penalti.

Kipa wa Uholanzi Tim Krul  aliyeingia uwanjani sekunde 44 kabla ya kumalizika kwa muda wa ziada aliokoa penalti mbili na kuifikisha timu yake katika hatua hiyo.

Hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana na Costa Rica kufika katika hatua ya robo fainali.

Mshambulizi wa Uholanzi  Arjen Robben akikabwa na wachezaji wa Costa Rica
Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben akikabwa na wachezaji wa Costa Rica FIFA.COM

Uholanzi sasa watamenyana na Argentina katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumatano juma lijalo, huku wenyeji Brazil wakipambana na Ujerumani siku ya Jumanne.

Fainali ni Jumapili iliyo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.