Pata taarifa kuu
BRAZIL 2014

Algeria yaifunga Korea Kusini mabao 4 kwa 2 kuweka matumaini ya kusonga mbele

Timu ya taifa ya Algeria imefufua matumaini ya Afrika kufanya vizuri katika michuano ya soka ya kombe la dunia  inayoendela nchini Brazil baada ya kuifunga Jamhuri ya Korea mabao 4 kea 2 Jumapili usiku.

Wachezaji wa Algeria wakisherekea bao
Wachezaji wa Algeria wakisherekea bao REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu umewawezesha Algeria kupanda hadi katika nafasi ya pili katika kundi lao wakiwa na alama 3, baada ya Ubelgiji ambao wana alama 6 na tayari wamefuzu katika hatua ya 16 bora kuifunga Urusi bao 1 kwa 0 Jumapilli usiku.

Mabao ya Algeria yalitiwa kimyani na Rafick Halliche, Abdelmoumene Djabou,Yacine Brahimi na Islam Slimani  huku mabao ya Korea ya kufuta machozi yakifungwa na Song Heung-min na  Koo Ja-cheol  kujaribu kusawazisha bila mafanikio.

Huu ndio ushindi wa kwanza wa Algeria katika michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982 na katika mchuano wa ufunguzi karibu wawafunge viongozi wa kundi hilo Ubelgiji.

Mashabiki wa Algeria
Mashabiki wa Algeria REUTERS/Damir Sagol

Algeria pia inakuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufunga mabao manne katika michuano hii ya kombe la dunia.

Mchuano wa mwisho wa vijana hao wa Desert Foxes utakuwa dhidi ya Urusi na ikiwa watashinda au kutoka sare na Ubelgiji kuifunga Korea Kusini watafuzu katika hatua ya 16 bora.

Kocha wa Algeria, Vahid Halilhodzic ambaye alikibadilisha kikosi chake katika mchuano huo amesema vijana wake walicheza kama alivyowaagiza licha ya kulegea katika kipindi cha pili.

Naye kocha wa Korea Kusini Hong Myung-bo amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wengi uwanjani na kuwaahidi ushindi dhidi ya Ubelgiji katika mchuano wake wa kwanza.

Mbali na mchuano huo, Ubelgiji wamejihakikishia nafasi ya 16 bora baada ya kupata ushindi katika mchuano wake dhdi ya Urusi.

Divock Origi mshambulizi wa Ubelgiji akifunga bao
Divock Origi mshambulizi wa Ubelgiji akifunga bao REUTERS/Alessandro Garofalo

Bao la pekee la Ubelgiji lilifungwa na mshambulizi Divock Origi mzaliwa wa Kenya ambaye aliingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Romelu Lukaku.

Mchuano mwingine wa kuvutia ulikuwa ni kati ya Marekani na Ureno ambao ulimazika kwa sare ya mbao 2 kwa 2.

 Louis Nani na Silvestre Varela ndio waliioifungua Ureno huku, Jermaine Jones na Clint Dempsey wakiifungua Marekani.

Mchezaji wa Ureno  Eder Kulia akimenyana na  Matt Besler wa Marekani
Mchezaji wa Ureno Eder Kulia akimenyana na Matt Besler wa Marekani Reuters/Dylan Martinez

Hakuna timu iliyofuzu katika kundi hilo, Ujerumani inaongoza kundi hilo kwa alama 4 ,Marekani ni ya pili kwa alama 4, Ghana wana alama moja huku Ureno wakiwa hawana alama.

Ghana itacheza na Ureno katika mchuano wake wa mwisho kusaka nafasi ya kufuzu katika mzunguko wa pili.

Jumatatu usiku, Cameroon watamenyana na Brazil katika mchuano wake wa mwisho kabla ya kurudi nyumbani kwa sababu wamefungwa katika mechi zao mbili, Croatia itapambana na  Mexico, Uhispania na Austaralia,  na Uholanzi na Chile.

Uhispania na Cameroon tayari wamebanduliwa nje ya michuano hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.