Pata taarifa kuu
Tanzania-Ligi kuu ya Vodacom

AZAM FC bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

AZAM FC ndiye bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine mjini Dar es Salaam, huku waliokuwa wapinzani wao katika mbio za taji hilo, Yanga SC wakishinda 2-1 dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha jana. 

Azam FC yaongoza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga  Mbeya City mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine mjini Dar es Salaam.
Azam FC yaongoza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine mjini Dar es Salaam. Azam FC
Matangazo ya kibiashara

Azam imefikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote baada ya mechi za mwisho aprili 19, mwaka huu. Yanga SC yenye pointi 55 sasa ikiifunga Simba SC Aprili wiki ijayo itafikisha 58.
Mabao ya Azam yamefungwa na Gaudence Mwaikimba na John Bocco, wakati bao la Mbeya City limefungwa na Mwagane Yeya.

Mchezo ulikuwa mkali na ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu, na sifa ziwaendee makipa wa timu zote mbili, David Burhan wa Mbeya City na Aishi Manula wa Azam FC kwa kazi nzuri ya kuokoa hatari langoni mwao.

Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 43, mfungaji Gaudence Mwakimba aliyemalizia pasi nzuri ya beki wa kulia Erasto Nyoni.

Baada ya bao hilo, Mbeya City walicharuka na kufanya mashambulizi mawili hatari langoni mwa Azam, lakini hawakuweza kupata bao hadi kipenga cha kuhitimisha kipindi cha kwanza kinapulizwa.

Kipindi cha pili, Azam waliingia na mfumo wa kucheza kwa kujihami ili kulinda bao lao, mbele wakimuacha Mwaikimbe pekee na John Bocco akashuka katikati huku Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akimsaidia Kipre Balou kukaba kiungo cha chini.

Mfumo huo ulikabirisha mashambulizi mengi langoni mwa Azam na haikuwa ajabu Mbeya City walipokomboa bao dakika ya 70 kupitia kwa Mwagane Yeya baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa na kipa Aishi Manula kufuatia shuti la Deus Kaseke.

Bao hilo kidogo liliwachanganya Azam FC na Mbeya City wakauteka mchezo kwa dakika kadhaa, kabla ya shambulizi la kushitukiza kuipa ushindi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa dakika ya 86, baadaa ya John Bocco kukutana na mpira uliorudishwa.

Wachezaji wa Mbeya City walimzonga refa Nathan Lazaro wa Kilimanjaro baada ya bao hilo na kusababisha mchezo kusimama kwa zaidi ya dakika tatu.

Refa huyo alitoa kadi nyekundu kwa Mwagane Yeya baada ya vurugu hizo.

Askari wa jeshi la Polisi walilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya mechi kwa kuwadhibiti mashabiki wa Mbeya City waliotaka kufanya vurugu na pia kuusindikiza msafara wa Azam FC.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.