rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Libya Ghana Nigeria Zimbabwe Afrika Kusini

Imechapishwa • Imehaririwa

Libya yatwaa ubingwa wa michuano ya CHAN mwaka 2014

media

Timu ya Taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika CHAN mwaka 2014 katika michuano iliyomalizika mwishoni mwa juma hili nchini Afrika Kusini.


Libya imetwaa taji hilo kwa kuifunga Ghana mabao 4-3 kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 za mtanange huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hili ni taji la kwanza la kimataifa katika mchezo wa soka kutwaliwa na Timu ya Taifa ya Libya kupitia michuano ya CHAN ambayo huwashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani pekee.

Matokeo hayo yameamsha shamrashamra za wapenzi wa soka katika mji mkuu wa Libya Tripoli ambapo mashabiki wamekesha mitaani wakishangilia ushindi huo.

Katika mchezo wa awali wa kusaka nafasi ya mshindi wa tatu, Nigeria iliifunga Zimbabwe bao 1-0 na kujinyakulia medali ya shaba ya michuano hiyo.