Pata taarifa kuu
LIGI KUU UINGEREZA

Uingereza : Arsène Wenger aongezwa muda wa kuendelea kuinoa Arsenal

Klabu ya Arsenal itapendekeza kuongezwa kwa kandarasi kwa meneja wake raia wa Ufaransa, Arsène Wenger, ambae muda wa kandarasi yake utakua umekwisha mwishoni mwa msimu, amethibitisha leo mkurugenzi mkuu wa klabu hio Ivan Gazidis. “Arsène ataendelea na sisi”, amesema Gazidis wakati wa kutiliana saini ya kandarasi mpya ya ufadhili kati ya Arsenal na kampuni Puma.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsène Wenger
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsène Wenger RFI
Matangazo ya kibiashara

“ Tumeridhika, na ikihitajika tuatoa tangazo tukifahamisha kwamba ni mtu bora kwetu” ameendelea kusema kiongozi huyo wa Arsenal, akibaini kwamba klabu hio ya Uingereza imekua ikimuunga mkono kwa jinsi anavyoiendeleza.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, kandarasi hio kati ya Arsenal na Puma ni ya euros milioni 36.7 kwa mwaka, sawa na pesa zinazotolewa na shirika la ndege la Emirates Airlines, ambalo ni mfadhili mkuu wa klabu ya Arsenal.

Arsenal ilimnunua mwaka uliyopita mchezaji wa klabu ya Ujerumani Real Madrid, Mesut Özil kwa euros milioni 50.

Wakati huohuo mshambuliaji kutoka Ufaransa, David Ngog aneichezea klabu ya Bolton nchini Uingereza katika daraja la pili, sasa amerejea katika daraja la kwanza, baada ya kujiunga tangu jana na klabu ya Swansea kwa kitita ambacho hakikutangazwa.

Kujiunga kwa mshamuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambae aliwahi kuichezea klabu ya Paris Saint-Germain, ni furaha kubwa kwa meneja wa klabu ya Swansea, Gallois Michael Laudrup, ambae amemkosa kwa kipindi kirefu mshambuliaji wake nyota Michu, ambae anauguza jeraha la mguu.

Ngog anakuja kuipa nguvu Swansea, baada ya kuonekana siku za hivi karibuni kua ni mshambuliaji mahiri katika klabu ya Bolton.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.