Pata taarifa kuu
Ufaransa

Mashindano ya Tour de France mwaka 2015 kuanzia nchini Netherlands

Shirika la maandalizi ya mashindano ya mbio za baiskeli ya Tour de France AmaurySports Organisation (ASO) leo Alhamisi limeweka wazi kuwa hatua ya ufunguzi wa mashindano hayo mwaka 2015 itakuwa ya majaribio ya mtu binafsi.

Waendesha baiskeli wakiwa kwenye mashindano ya Tour de France
Waendesha baiskeli wakiwa kwenye mashindano ya Tour de France commons.wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Tayari shirika hilo limetangaza kuwa mashindano hayo kwa mwaka 2015 yataanzia huko Utrecht nchini Netherlands.

Naye mkurugenzi wa mashindano Christian Prudhomme ametangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye makao ya balozi wa Uholanzi nchini Ufaransa Ed Kronenburg kwamba mbio hizo za majaribio za umbali wa kilomita 13.7 zitaanza Jumamosi tarehe 4 mwezi Julai.

Hatua ya pili itaanza siku ya Jumapili Julai 5 huko Utrecht kabla ya kuelekea nyumbani nchini Ufaransa siku moja baadaye.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.