Pata taarifa kuu
BAISKELI

Armstrong: Niko tayari kutoa ushahidi wa wazi iwapo nitatendewa haki

Mwendesha baiskeli, Lance Armstrong ambaye hivi karibuni alinyang'anywa taji lake Tour de France la mwaka 2012 baada ya kubainika kutumia dawa za kusisimua misuli, amesema atashirikiana na tume maalumu iliyoundwa kuchunguza wanamichezo wanaotuhumiwa kutumia dawa hizo.

Mwendesha baiskeli, Lance Armstrong ambaye hivi karibuni alikiri kutumia dawa za kusisimua misuli
Mwendesha baiskeli, Lance Armstrong ambaye hivi karibuni alikiri kutumia dawa za kusisimua misuli Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sakata la Armstrong ambalo lilizua mjadala mkubwa duniani hasa kwa wanamichezo ambao wamekuwa na tabia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, limekuwa ni tukio la mfano kwa wanamichezo wengi ambao sasa wanahofia kutumia dawa hizo.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha televisheni cha nchini Uingereza, Armstrong amesema atashirikiana na shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli mchezoni.

Mchezaji huyo akaongeza kuwa, atafanya hivyo iwapo taasisi hiyo itatenda haki wakati wa yeye anapotoa ushahidi wake wakati huu ambapo mwezi January mwaka huu alikiri kuwa mara kadhaa alikwepa upimaji iwapo alitumia dawa za kusisimua misuli au la.

Armstrong ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ambayo imechukuliwa dhidi yake huku akisema baadhi ya wakimbiza baiskeli wengine ambao wanatumia dawa na wamekuwa wakitumia wanaachwa huku wachache wakipewa adhabu kali maishani mwao.

Armstrong alitajwa na shirika la Marekani linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli, likimtaja kama mmoja wa wachezaji waliofanikiwa mara nyingi zaidi duniani kukwepa mtego wa kupimwa kubaini iwapo walitumia dawa za kusisimua misuli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.