Pata taarifa kuu
SOKA-UINGEREZA

Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic ataka wachezaji kurejea kwenye kiwango chao ili kupata matokeo mazuri

Nahodha wa Klabu wa Manchester United Nemanja Vidic ametoa wito kwa wachezaji wenzake kuhakikisha wanarejea kwenye hali yao ya kawaida ili waweze kufanya vizuri kwenye mchezo Ligi Kuu dhidi ya Sunderland na kusahau matokeo mabaya waliyopitia. Vidic amesema hatua ya wachezaji kurudi kwenye hali yao ya kawaida itasaidia kupunguza shinikizo linalomkabili Kocha Mkuu David Moyes aliyeshuhudia vichapo viwili mfululizo kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza.

Nahodha wa Mabingwa Watetezi Nchini Uingereza Klabu ya Manchester United Nemanja Vidic
Nahodha wa Mabingwa Watetezi Nchini Uingereza Klabu ya Manchester United Nemanja Vidic
Matangazo ya kibiashara

Manchester United inashika nafasi ya kumi na mbili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kufungwa na Manchester City kabla ya kupata kichapo cha nyumbani mbele ya West Bromwich Albion.

Klabu hiyo imejikuta kwenye nafasi ya kumi na mbili kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kuonekana imepata matokeo mabaya zaidi tangu ishuhudie mwanzo mbaya kama huo mnamo mwaka 1989.

Vidic amewataka wachezaji wote kukuabaliana na hali halisi kwamba hawajaanza msimu vizuri mwaka huu kitu ambacho kimeshusha morali ya baadhi ya wachezaji na kuanza kuingiwa na hofu.

Nahodha huyo ameweka bayana klabu haijashuhudia kiwango ambacho wamekuwa wakikihitaji ndiyo maana wamekuwa na matokeo mabaya lakini iwapo wachezaji watajenga kujiamini mambo yatakuwa mazuri.

Beki huyo wa kati wa Timu ya Taifa ya Serbia amesema bado kikosi hicho kinawachezaji mahiri kabisa hivyo ni suala la muda tu kabla hawajarejesha kujiamini kulikoonekana kupotea kwa sasa.

Vidic amekiri wamekumbana na matokeo ya kukatisha tamaa baada ya kufungwa michezo mwili ya Ligi Kuu nchini Uingereza na hivyo kuwafanya kupoteza michezo mitatu kati ya sita waliyocheza.

Manchester United inarejea kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza jumamosi hii dhidi ya Sunderland ikiwa na kumbukumbu za kupata sare kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Shakhtar Donetsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.