rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza Roy Hodgson

Imechapishwa • Imehaririwa

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza Hodgson asema tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2014 ipo mikononi mwao

media
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Roy Hodgson

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Roy Hodgson ametamka wazi anauhakika kikosi chake kitafanikiwa kukata tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.


Hodgson amesisitiza Uingereza ina nafasi ya kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka 2014 iwapo itashinda michezo yake miwili ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Brazil.

Kocha huyo wa Timu ya Taifa ya Uingereza amesema kwa sasa amekuwa akiangalia kwa karibu mno michezo yao miwili ya kufuzu Kombe la Dunia itayopigwa baada ya juma moja ili kusaka tiketi hiyo muhimu.

Timu ya Taifa ya Uingereza inatarajiwa kucheza michezo miwili katika ya Montenegro na Poland iliyopangwa kufanyika tarehe 11 na 15 na iwapo itashinda michezo hiyo miwili itakuwa imejipatia tiketi hiyo muhimu.

Uingereza inaongoza Kundi H ikiwa na pointi kumi na sita baada ya kucheza michezo nane na kufuatiwa kwa karibu na Ukraine inayoshika nafasi ya pili ikiwa imeachwa kwa pointi moja sawa kabisa na Montenegro.

Hodgson ameweka bayana anaamini wachezaji wake hawatapoteza nafasi hiyo iliyopo kwenye mikono yao na iwapo watashindwa kutumia fursa hiyo basi hawatapaswa kumsaka mchawi aliyechangia kukosa tiketi hiyo.

Kocha Hodgson amesema ameanza kuelekeza mawazo yake kwenye mchezo dhidi ya Montenegro utakaopigwa siku ya Ijumaa ya juma lijalo kabla ya jumanne kuwa na kibarua kingine mbele ya Poland.