rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Misri Uganda Milutin Micho Sredojevic Bob Bradley

Imechapishwa • Imehaririwa

Timu ya Taifa ya Misri yaendelea kushusha kichapo kwa Uganda kwenye michezo yake miwili ya kirafiki

media
Beki wa Timu ya taifa ya Uganda akikabiliana na mshambuliaji wa Misri kwenye mchezo wa kirafiki

Timu ya Taifa ya Uganda imeendelea kuwa vibonde vya kudumu mbele ya Misri baada ya kukabali kichapo cha pili kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyofanyika katika kipindi cha siku tatu.


Pharaohs waliendeleza ubabe mbele ya Cranes baada ya kuwachakaza kwa jumla ya magoli 3-0 katika mchezo wa pili wa kirafiki wa kujiandaa na hatua ya mtoano dhidi ya Ghana kusaka tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Mapema jumatatu Uganda ilipata kichapo cha magoli 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kirafiki ambapo magoli ya Pharaohs walifanikiwa kuonesha kandanda ya kuvutia kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Jeshi.

Magoli ya Timu ya Taifa ya Misri kwenye mchezo huo wa kirafiki yaliwekwa kimiani na Ahmed Eid, Mohamed Abdul Shafy kabla ya Ahmed Samir hajatamatisha karamu yao ya magoli.

Timu ya Taifa ya Misri imeshafanikiwa kushinda michezo mitatu ya kirafiki waliyocheza mwaka huu ambapo kwenye mchezo wa kwanza Pharaohs walivuna ushindi wa magoli 3-0 kwenye mchezo uliopigwa katika Jiji la El Gouna mwezi Agosti.

Kwenye mchezo huo wa kirafiki Uganda walikosa penalti iliyopigwa na Brian Majwega na hivyo kuodnoka nchini Misri wakiwa hawajafunga goli lolote kwenye michezo hiyo miwili ya kirafiki.

Kocha Mkuu wa Cranes Milutin Micho Sredojevic amekiri kufurahishwa na namna ambavyo wachezaji wake walivyocheza kwenye michezo hiyo miwili ya kirafiki iliyopigwa huko Cairo.

Misri ikiwa chini ya Bob Bradley imetumia michezo yake miwili ya kirafiki dhidi ya Uganda kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao na Ghana huku Cranes wakijiandaa kwa mashindano ya CECAFA yatakayofanyika mwezi ujao na CHAN itakayofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.