Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Barcelona yaendelea kung'ara katika ligi kuu ya soka Uhispania

Bosi wa klabu ya soka ya Barcelona Gerardo Martino, ameeleza kufurahishwa na kiwango cha wanasoka wake kilichowapatia ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Real Sociedad katika mechi ya jana jumanne ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka ya nchini Uhispania La Liga.

REUTERS/Alejandro Guerrero
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo wa nyumbani katika dimba la Camp Nou umeendelea kuing'arisha Barca iliyopo kileleni ikiwa na alama 18 ifuatiwa na Atletico de Madrid wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Real Madrid.

Mabao ya awali yaliyopachikwa nyavuni na Neymar, Lionel Messi na Sergio Busquets yaliiwezesha Barca kung'ara baada ya kutamatika nusu ya kwanza ya kipindi cha mchezo huo.

Martino amesema atahakikisha wanatumia mbinu zaidi kujakikisha wanaendelea kusalia nambari moja katika msimamo na tayari amebainisha kuwa ataendelea na sera yake ya mzunguko na kuwapumzisha baadhi ya nyota wa klabu hiyo.

Kwa hiyo Messi na Neymar hawatakuwapo katika mchuano wa nusu fainali ili waweze kurejea hapo baadaye kabla katika fainali.

Matokeo mengine ya mechi za La Liga zilizotimua vimbi hiyo jana ni ushindi wa Atletico de Madrid wa 2-1 dhidi ya Osasuna, Mlaga waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Almera na Levante walitoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Real Valladolid.

Mitanange inayotarajiw akushuhudiwa hii leo ni kati ya Sevilla na Rayo Vallecano, Granada FC na Valencia wakati Real Madrid itakuwa na kibarua dhidi ya Elche.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.