Pata taarifa kuu
SOKA

Kocha Mpya wa Barcelona Gerardo Martino akiri ushawishi wa Lionel Messi ndiyo umechangia kuteuliwa kwake kuwa Mrithi wa Vilanova

Kocha Mpya wa Mabingwa wa Uhispania Barcelona Gerardo Martino maarufu kwa jina la Tata amekiri uhusiano wake mzuri na Mchezaji Bora wa Duniani Lionel Messi ndiyo umechangia yeye kupata nafasi ya kumrithi Tito Vilanova.

Kocha Mpya wa Barcelona Gerardo Martino
Kocha Mpya wa Barcelona Gerardo Martino
Matangazo ya kibiashara

Martino ambaye ni rais wa Argentina kama alivyo Messi anatajwa kukabidhiwa jukumu la kuinoa Barcelona baada ya mchezaji huyo wa Dunia kushinikiza kupewa kazi hiyo baada ya Vilanova kutangaza kujiuzulu kutokana na sababu za kiafya.

Kocha huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Paraguay amekiri hailewi nini kilichangia yeye kupewa kazi hiyo lakini anaamini ushawishi uliofanywa na Messi pamoja na babake Jorge ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa yeye kuwa Kocha Mpya.

Martino mwenye umri wa miaka 50 amesema ni lazima watu hao wawili waliulizwa maoni yao juu ya kocha ajaye na hivyo wao wakampendekeza yeye kutokana na kufahamu kazi yake vilivyo.

Kocha huyo amewaambia wanahabari waliokusanyika huko Rosario kwamba kwake ilikuwa ni kitu cha kushangaza kuambiwa amechaguliwa kuwa Kocha Mkuu wa Barcelona na sasa anaanza kuangalia ni kwa namna gani atafanyakazi yake ipasavyo.

Martino aliyekuwa anainoa Klabu ya Newell's Old Boys amewaambia wanahabari pia benchi lake la ufundi litakuwa tayari kuendelea kumsaidia Messi ili aweze kuendelea kuwa bora zaidi katika siku za baadaye.

Kocha huyo pia anatarajiwa kuanza kazi rasmi ya kuinoa Barcelona hiyo kesho baada ya hii leo kucheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich ikiwa ni sehemu ya maandilizi ya msimu ujao.

Martino kwenye benchi lake la ufundi atakuwepo na Adrian Coria ambaye anakumbukwa sana kwenye juhudi za kumuibua messi akiwa kwenye timu ya watoto wenye umri wa miaka 13 katika Klabu ya Newell's.

Kocha Mpya wa Barcelona Martino ameingia mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo huku akiwa anaingia kwenye rekodi kutokana na kutowahi kufundishi klabu yoyote Barani Ulaya hapo kabla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.