Pata taarifa kuu
RIADHA

Wanariadha Asafa Powell na Tyson Gay wabainika kutumia dawa za kusisimua misuli

Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 raia wa Marekani, Tyson Gay na mwenzake wa Jamaica Asafa Powell wamejikuta kwenye matatizo baada ya kubainika kuwa walitumia dawa za kusisimua misuli kwenye mashindano mbalimbali waliyoshiriki.

Mwanariadha, Asafa Powell (kushoto) na mwenzake Tayson Gay (Kulia) ambao wote wamebainika kutumia dawa za kusisimua misuli
Mwanariadha, Asafa Powell (kushoto) na mwenzake Tayson Gay (Kulia) ambao wote wamebainika kutumia dawa za kusisimua misuli Reuters
Matangazo ya kibiashara

Gay ambaye anajumuishwa kwenye nafasi ya pili duniani katika mbio za mita 100 ameambiwa na shirika la Marekani linalochunguza iwapo wachezaji wametumia dawa za kusisimua misuli, kuwa damu yake imeonesha kuwa alitumia dawa hizo kwenye mashindano ya mwezi May.

Kwa matokeo hayo sasa ni wazi Gay anasubiri uamuzi wa shirikisho la riadha la dunia iwapo litamchukulia hatua au la jambo ambalo limeonekana kuwakera mashabiki wake.

Kwa upande wake Asafa Powell yeye pia imebainika kuwa alitumia dawa za kusisimua misuli kwenye mashindano ya mwezi June yaliyofanyika nchini mwake na kumuweka kwenye wakati mgumu kuhusu hatma yake.

Mwanariadha mwingine wa Jamaica Sherone Simpson nae alibainika kutumia dawa za kusisimua misuli kwenue mashindano hayohayo ya Jamaica wakati akishiriki mbi za mita 400 za kupokezana vijiti.

Powell ndiye alikuwa mwanariadha pekee anaeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mia 100 kabla ya rekodi yake kuvunjwa na mwanariahda mwenzake wa Jamaica Usain Bolt mwaka 2008.

Gay ametoa taarifa kukanusha kuwa alitumia dawa hizo kwa makusudi na kwamba anaomba radhi kwa mashabiki wake na shirikisho la riadha la dunia kwakuwa hakufanya makusudi.

Wanariadha wote hawa wenye majina makubwa wanasubiri uamuzi wa mashrikisho yao ya raidha kwenye zao iwapo watachukuliwa hatua au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.