Pata taarifa kuu
RIADHA

Usain Bolt aweka rekodi mpya katika mbio za mita 200

Bingwa wa michezo ya Olimpiki katika mbio za mita 100 na 200 kwa upande wa wanaume Mjamaica Usain Bolt aliweka rekodi mpya katika mbio za Mita 200 wakati wa mashindano ya kimataifa ya Oslo Diamond League kwa kumaliza kwa muda wa sekunde 19 nukta 17.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu wa Bolt unakuja wiki moja baada ya kushindwa kutamba katika mbio za mita 100 mbele ya Mmarekani Justin Gatlin jijini Rome Italia katika mashindano hayo ya Kimataifa ya shirikisho la riadha duniani la IAAF.

Mbio hizo za Alhamisi zilimwazia vibaya Bolt baada ya mwanaridha kutoka Uholanzi Churandy Martina, kuingia katika mstari wake  na kumtatiza.

Saidy Ndure kutoka Norway alimaliza wa pili kwa muda wa sekunde 20 nukta 36 huku James Ellington kutoka Uingereza akimaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa sekunde 20 nukta 55.

Bolt amesema kuwa hali yake ni nzuri licha ya kushindwa wiki iliyopita na huo  umemwezesha kuvunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha Frank Fredericks kutoka Namibia  mwaka 1996 aliyetumia muda wa sekunde 19 nukta 82.

Katika mbio zingine,  bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 5,000 kwa upande wa akina wa wanawake alishinda mbio hizo kwa muda wa dakika 14 sekunde 15 nukta 75 nyuma ya Mwiethiopia mwenzake Tirunesh Dibaba.

Katika mbio za 3,000 kuzuka maji na viuzi, wakenya waliendeleza ushindi wao baada ya chipukiizi Conseslus Kipruto mwenye umri wa miaka 19 kunyakua ushindi kwa muda wa dakika 8 sekunde 4 nukta 48 huku nafasi ya pili ikimwendea bingwa wa Olimpiki Ezekiel Kembo huku Hillary Kipsang Yego akifunga tatu bora.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.