Pata taarifa kuu
TENNIS

Rafael Nadal aweka historia katika michuano ya French Open

Rafael Nadal ameweka historia katika mchezo wa Tennis kwa kushinda taji lake la  nane la French Open Jumapili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Nadal mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uhispania aliweka historia hiyo ya michuano ya French Open kwa kumgaragaza mwenzake David Ferrer pia kutoka Uhispania kwa seti za 6-3, 6-2, 6-3.

Nadal amesema hawezi kuamini kuwa amefanikiwa kuweka historia katika michuano hiyo jijini Paris hasa baada ya kuuguza jeraha kwa muda wa miezi saba .

Mchezaji huyo aliyelemewa na machozi ya furaha jijini Paris aliongeza kuwa hakuamini macho yake kuona amepata ushindi huo mkubwa baada ya kuondolewa katika mashindano makubwa ya Wimbledon mwaka uliopita.

Jeraha la Nadal lilimsababisha kukosa michuano ya Olimpiki mwaka uliopita ,pamoja na yale ya US na Australian Open.

Ushindi huo sasa unamfanya kuwa na jumla ya mataji 12 makuu sawa na Roy Emerson na sasa analenga kuvunja rekodi ya Roger Federer ambaye ana jumla ya mataji 17 makuu.

Kati ya michuano 60 alizocheza jijini Paris, Nadal amefanikiwa kushinda mechi 59 na kuwa mchezaji mwenye rekodi bora nchini Ufaransa.

Kwa upande wa akina dada, Mmarekani Serena Williams alimshinda mchezaji bora duniani Maria Sharapova kutoka Urusi kwa seti za 6-4, 6-4 ushindi wake wa kwanza wa French Open tangu mwaka 2002.

Serena Williams kwa ujumla sasa ameshinda mataji 16 .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.