Pata taarifa kuu
SOKA

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Namibia ajiuzulu

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Namibia Roger Palmgren amejiuzulu siku moja kabla ya timu hiyo kuikaribisha Nigeria jijini Windhoek katika mchuano wa kutafuta tiketi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Palmgrena raia wa Sweden, ameliambia shirikisho la soka nchini humo kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuhofia usalama wake jijini Windhoek baada ya kudai kuwa alitishwa wiki mbili zilizopita akiwa hotelini mwake.

Aidha, kocha huyo ameeleza kuwa amekuwa akihofia usalama wake tangu mwezi Mei wakati Namibia  ilipotoka sare ya kutofunga na Zambia katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki.

Mchuano wa Namibia Jumatano ilyopita jijini Blantyre ulimalizika kwa timu zote kupata sare ya kutofungana matokeo ambayo kocha huyo anasema huenda yakamletea matatizo kutokana na hasira za mashabiki wa soka nchini humo.

Viongozi wa soka nchini humo wanasema wamekuwa wakimshuku kocha huyo kuwa na mpango wa kuondoka ili kujiunga na aliyekuwa wakati mmoja mkufunzi wa Uingereza Sven Goran Eriksson, ambaye amepata kazi nchini China.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Santos Ricardo Mannetti ameteuliwa na viongozi wa soka nchini humo kuwa mkufunzi wa muda, kukinoa kikosi hicho kumenyana na Nigeria Jumatano usiku katika uwanja wa Kimataifa wa Sam Nujoma.

Namibia ambayo iko katika kundi moja na Nigeria, Malawi na Kenya ni ya tatu kwa alama 4 na matumaini yake ya kusonga mbele katika duru ya mwisho ya kusaka tiketi ya kuelekea kombe la dunia yamedidimia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.