Pata taarifa kuu
FIFA-MAURITIUS

Mkutano mkuu wa FIFA wapitisha sheria mpya za kukabiliana na vitendo vya kibaguzi uwanjani

Mkutano mkuu wa shirikisho la kabumbu duniani FIFA unaofanyika nchini Mauritius hii leo kwa kauli moja umeazimia na kupitisha sheria mpya zinazokataza vitendo vya kibaguzi uwanjani. 

FIFA hivi karibuni imeamua kupendekeza kutungwa kwa sheria maalumu kukabiliana na vitendo vya kibaguzi mchezoni
FIFA hivi karibuni imeamua kupendekeza kutungwa kwa sheria maalumu kukabiliana na vitendo vya kibaguzi mchezoni Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe 204 walipiga kura kuunga mkono mabadiliko ya sheria hizo mpya huku kura moja ikisema hapana katika zoezi ambalo lilihitaji wajumbe 207 kushiriki kwenye upigaji wa kura.

Sheria hizo mpya zilizobuniwa na kamati maalumu ya FIFA ya kupambana na vitendo vya kibaguzi uwanjani, inataka iwapo mtu akipatikana na hatia apewe onyo, alipe faini ama adhabu kali ichukuliwe dhidi yake kutokana na ishara hizo.

Sehemu ya pili ya sheria hiyo inataka mtu aliyepatikana na hatia ya kutenda kosa hilo apunguziwe alama ama atolewe kwenye mashindano ama ligi kuu kwa lengo la kukabiliana na vitendo hivyo.

Sheria hiyo imeongeza kuwa kwa mchezaji, afisa wa FIFA ama mwamuzi ambaye atapatikana na hatia ya kutenda kosa hilo atafungiwa angalau mecho tano pamoja na kufungwa kwa uwanja ambao mashabiki wake watakuwa wameonesha vitendo vya kibaguzi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ameonya kuwa sheria hizo mpya zilizopitishwa hazitabagua mtu yeyote wala afisa wa FIFA ambaye atabainika kutoa ishara za kibaguzi uwanjani.

Akizungumza nchini Mauritius ambako mkutano wa mwaka wa FIFA unafanyika, mwenyekiti huyo amesema vikwazo vipya dhidi ya vitendo vya kibaguzi vitahusu hata nchi waandaaji wa kombe la dunia katika miaka ijayo iwapo wachezaji ama vilabu vyake vitakithiri kwa vitendo vya kibaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.