Pata taarifa kuu
ITALIA-SERIE A

Mario Balotelli ni miongoni mwa Wachezaji wanaoshinikiza Kocha Massimiliano Allegri aendelea kuinoa AC Milan msimu ujao

Kocha Mkuu wa AC Milan Massimiliano Allegri ameendelea kupigiwa chapuo ya kuendelea kusalia kukinoa kikosi hicho katika msimu ujao licha ya kupata matokeo mabaya msimu huu na kushindwa kutwaa taji lililotetewa na Juventus.

Kocha Mkuu wa AC Milan Massimiliano Allegri akimpa maelezo Mshambuliaji wake Mario Balotelli
Kocha Mkuu wa AC Milan Massimiliano Allegri akimpa maelezo Mshambuliaji wake Mario Balotelli
Matangazo ya kibiashara

AC Milan inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A ikiwa na juma ya pointi sitini na tano nyuma ya Napoli wenye pointi sabini na mbili huku michezo mitatu pekee ikisalia kabla ya kumalizika kwa ligi msimu huu.

Wachezaji wa AC Milan wanaona kuwa Kocha Allegri anapaswa kuendelea kupewa nafasi zaidi ya kundelea kusalia kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao na wana uhakika hiyo itasaidia kushinda Ligi ya Serie A msimu ujao.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia Mario Balotelli ndiye amekuwa mchezaji wa hivi karibuni kumtetea Allegri aendelee kusalia kuwa Kocha Mkuu ili aweze kuendelea kazi nzuri aliyoanza kuifanya kwa timu hiyo.

Balotelli amesema wachezaji wamekuwa wakifurahia uwepo wa Kocha Allegri hivyo haoni sababu ya kutimuliwa licha ya timu hiyo kushindwa kutwaa taji hilo lililowaponyoka miaka miwili iliyopita.

Wachezaji wameanza kumtetea Allegri mwenye umri wa miaka 45 baada ya uwepo wa taarifa za kupendekezwa kwa wachezaji wa zamani Clarence Seedorf na Mark Van Bommel wapewe kazi ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao.

Haya yanakuja kipindi hiki ambacho Kocha Allegri amekiri kufurahishwa na namna wachezaji wake walivyopigana na kufanikiwa kuzoa pointi 41 kwenye mzunguko wa pili wa Ligi ya Serie A.

Allegri amekiri katika kipindi cha miaka 26 AC Milan imekuwa kwenye nafasi za juu lakini hali ilikuwa tofauti msimu huu kutokana na kuanza vibaya na kujikuta wakipoteza pointi nyingi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.