Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Sunderland imemtangaza Paolo Di Canio kuwa Kocha Mkuu baada ya kumtimua O'Neill kufuatia kupata matokeo mabaya

Uongozi wa Klabu ya Sunderlandy ya nchini Uingereza imemtangaza Paolo Di Canio kuwa Kocha Mkuu akichukua nafasi ya Martin O'Neill aliyetimuliwa baada ya timu hiyo kupata kichapo kutoka kwa Manchester United siku ya jumamosi. Di Canio ameingia mkataba wa miaka miwili na nusu ya kuinoa Sunderland kipindi hiki timu hiyo ikipigana kufa na kupona kujiepusha na baa la kushuka daraja kwani ipo karibu kabisa na eneo la timu tatu zinzoweza kushuka daraja.

Kocha Mkuu Mpya wa Sunderland Paolo Di Canio ambaye anaanza kibarua cha kuinoa Timu hiyo hii leo
Kocha Mkuu Mpya wa Sunderland Paolo Di Canio ambaye anaanza kibarua cha kuinoa Timu hiyo hii leo
Matangazo ya kibiashara

Di Canio raia wa Italia ambaye amekuwa mtukutu tangu akiwa mchezaji anachukua jukumu lililomshinda O'Neill na anaanza kutekeleza kibarua chake hii leo huku Uongozi wa Sunderland ukiamini ataiokoa klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Sunderland ndiyo ilithibitisha jukumu la kuionoa timu hiyo inayokabiliwa na matokeo mabaya limeachwa kwenye mikono ya Di Canio kutoka kwa O'Neill aliyebwagiwa manyanga.

Sunderland inakuwa klabu ya mbili kwa Di Canio tangu ameanza kazi ya ukocha na anachukua jukumu la kuingia kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza akitoa daraja la tatu alikokuwa anaifundisha Swindon Town.

Mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short amesema wanaimani na Di Canio kutokana na ari aliyonayo hivyo licha ya changamoto zilizombele yake lakini wanaamini ataweza kutimiza matarajio ya Uongozi na mashabiki.

Short amesema wamevutiwa na sana na uvumivu ambao umeoneshwa na mashabiki wa Sunderland ndiyo maana wao wamelazimika kuchukua jukumu la kuikoa timu hiyo isiteremke daraja.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Swindon Town Jeremy Wray amesema kuchukuliwa kwa Kocha wao ni hatua ya kuaminika kwa Di Canio kutokana na kazi nzuri ambayo ameifanya na wao wanamtakia kila la kheri.

Di Canio mwenye umri wa miaka 44 tangu amegeukia ukocha ameweza kuongoza michezo 95 huku akishinda 54 kwenda sare mara 18 na kushuhudia kikosi chake kikipoteza michezi 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.