Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha Pardew bado ana imani ya kuingia mkataba mpya na Mshambuliaji wake Demba Ba

Kocha Mkuu wa Newcastle United Alan Pardew ameeleza matumaini yake kwa mara nyingine ya kusalia na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal Demba Ba ambaye hatima yake haijajulika bado.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal na Klabu ya Newcastle United Demba Ba
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal na Klabu ya Newcastle United Demba Ba
Matangazo ya kibiashara

Pardew amesema bado hajafahamu kama Ba atasalia kuwepo Newcastle au la lakini kwa upande wake anaendelea kupambana kwa kila hali kuhakikisha anambakiza mshambuliaji huyo kwa kipindi zaidi.

Kocha Mkuu Pardew anasema kitu kikubwa kwa sasa ni kuafikiwa kwa mkataba mpya na Ba kitu ambacho kitakuwa ni ushindi kwa Klabu ya Newcastle kubakisha kwa ajili ya msimu huu na misumu ijayo.

Kauli ya Pardew inakuja huku taarifa zikienea mwakilishi wa mshambuliaji huyo kuanza mazungumzo na Chelsea siku ya jumapili lengo likiwa ni kunasa saini yake ili kuimarisha kikosi chao.

Pardew amesema yote kwa yote uamuzi wa mwisho utakuwa ni kwa Ba mwenyewe kama atahitaji kuendelea kusalia Newcastle au ataendelea kushikilia msimamo itakuwa ni vigumu kuendelea kuwa naye.

Kocha Mkuu wa Newcastle pia ameonekana kuhitaji zaidi uwepo wa Ba kwenye timu yake ambayo inapambana kwa kiwango cha hali ya juu kujiimarisha baada ya kuwa na msimu mbaya tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

Ba amefunga magoli 13 katika michezo 21 ambayo amecheza akiwa na Newcastle United na kuisaidia vilivyo timu hiyo licha ya kuwa katika nafasi za juu kama ilivyokuwa kwenye msimu uliopita uliokuwa wa mafanikio kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.