Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

John Terry atangaza kutundika daruga kucheza soka la kimataifa

Nahodha wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza John Terry hatimaye ametangaza kutundika daruga kucheza soka la kimataifa huku akikabiliwa na tuhuma za kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand.

Mchezaji wa Chelsea John Terry akionekana kujibizana na Anton Ferdinand mchezaji wa QPR
Mchezaji wa Chelsea John Terry akionekana kujibizana na Anton Ferdinand mchezaji wa QPR Reuters
Matangazo ya kibiashara

Terry mwenye umri wa miaka 31 hivi sasa ametangaza azma yake hapo jana kwa madai kuwa anaona muda umefika kupisha uchunguzi dhidi yake na kwamba kwa nia njema ya kutaka kutunza heshima yake ameamua kustaafu soka la kimataifa.

Uamuzi wa John Terry umeonekana kuwashtua mashabiki wengi wa soka nchini Uingereza kwakuwa hawakutarajia kuona mchezaji huyo akistaafu sasa punde baada ya kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa na kocha Roy Hodgson.

Terry anatangaza kustaafu soka wakati muda huu kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Uingereza FA inakutana kujadili hatma ya mchezaji huyo kuhusu tuhuma za kumtolea maneno ya kibaguzi beki wa QPR Anton Ferdinand.

Awali mahakama ya mjini Londo ilimkuta hana hatia ya kutoa matamshi hayo kwa madai kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu uthibitisho wa matamshi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.