Pata taarifa kuu
SOKA-OLIMPIKI

Wawakilishi wa Afrika Misri,Senegal hoi Olimpiki

Wajumbe wa bara la Afrika katika mchezo wa soka kwa upande wa wanaume timu ya Senegal na Misri wamejikuta wakitupwa nje ya michuano ya Olimpiki inayoendelea jijini London.

Mpambano kati ya Senegal na Mexico kama wachezaji wanavyoonekana pichani
Mpambano kati ya Senegal na Mexico kama wachezaji wanavyoonekana pichani REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Senegal na Misri ni timu pekee za Afrika zilizosalia hatua ya robo fainali ambapo jumamosi zilijikuta zikipokea kipigo cha mbwa mwizi ambapo awali Misri ilifungwa na Japan mabao 3-0 huku Senegal iliyotazamiwa kufanya vema ikiambulia kipigo cha magoli 4-2
toka kwa Mexico.

Senegal ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuwafunga Uruguay bao 2-0 na kutoa dalili za matumaini katika mchezo wa jumamosi baada ya kusawazisha mabao mawili kupitia Moussa Konate na Brahima Balde kabla ya Mexico kuvamia nyavu dakika ya 90 na katika muda wa nyongeza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.