Pata taarifa kuu
PALESTINA-MAREKANI-UNSC-USALAMA

Maandamano ya kumuunga Abbas yafanyika kabla ya hotuba yake mbele ya Baraza la Usalama

Maelfu ya Wapalestina wameandamana leo Jumanne katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza dhidi ya mpango wa Marekani wa kumaliza mzozo kati ya Israel na Palestina ambao Rais Mahmoud Abbas atapinga baadaye katika hotuba yake mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wapalestina wakiandamana kupinga mpango wa amani wa Marekani kwa Mashariki ya Kati Februari 11, 2020 katika mji wa Ramallah.
Wapalestina wakiandamana kupinga mpango wa amani wa Marekani kwa Mashariki ya Kati Februari 11, 2020 katika mji wa Ramallah. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wizi wa karne hii", "Palestina sio ya kuuza", "Tunatupilia mbali mpango wa karne hii", maneno ambayo yaliandikwa kwenye mabango yaliyokuwa yaliyokuwa yakionyeshwa na waandamanaji katikati mwa mji wa Ramallah, makao makuu ya Mamlaka ya Palestina ya Mahmoud Abbas

Watu wasiopungua 5,000 wamekusanyika katika mji wa Ukingo wa Magharibi kupinga mpango wa Marekani, uliopewa jina katika mitaa ya Palestina wakiuita "Safqat al-Qaran", "mpango wa karne hii," kwa mujibu wa waandishi wa habari wa shirika la Habari la AFP waliokuwa kwenye eneo la tukio.

Haya ni maandamano makubwa yaliyofanyika kwenye ardhi ya Palestina kuunga mkono Mahmoud Abbas katika miaka ya hivi karibuni na dhidi ya mpango wa Marekani, uliyotangazwa Januari 28 huko Washington na Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.