Pata taarifa kuu
ULAYA-MASHARIKI YA KATI-USALAMA

Ujumbe wa Ulaya wa ulinzi wa Mlango wa Hormuz wapanuka

Ufaransa, Denmark, Ugiriki na Uholanzi, nchi zinazoshiriki katika ujumbe wa majini wa ulinzi wa Mlango wa Hormuz, umepata "uungwaji mkono wa kisiasa" kutoka Ujerumani, Ubelgiji, Italia na Ureno.

Helikopta ya kijeshi ikitoa ulinzi kwa meli ya mafuta kwenye bahari ya Ghuba ikitokeq Mlango wa Hormuz, Desemba 21, 2018.
Helikopta ya kijeshi ikitoa ulinzi kwa meli ya mafuta kwenye bahari ya Ghuba ikitokeq Mlango wa Hormuz, Desemba 21, 2018. © REUTERS/Hamad I Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa nchini Ufaransa na Quai d'Orsay, nchi hizo nane zinasisitiza kwamba "hali ya sasa katika Ghuba na katika Mlango wa Hormuz bado haijabadilika katika eneo muhimu kwa utulivu duniani".

"Kwa kuunga mkono hoja ya kupunguka kwa maswala ya usalama wa kikanda", nchi hizo zimeongeza kuwa zimetoa "uungwaji wao mkono wa kisiasa kwa ajili ya kuunda ujumbe wa nchi za Ulaya kwa Uchunguzi wa baharini kwenye Mlqngo wa Hormuz (EMASOH)".

Nchi hizo pia zimebaini kwamba zimefurahishwa na ahadi mpya za kufanya kazi "katika siku zijazo" sambamba na Ufaransa, Denmark, Ugiriki na Uholanzi.

Mwezi Desemba mwaka jana Ufaransa ilitangaza kwamba itapeleka chombo kiitwacho Courbet kama sehemu ya ujumbe huu wa usalama.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini Ufaransa, ambayo ina kambi ya wanamaji huko Abu Dhabi, katika Falme za Kiarabu, nchi kadhaa za Ulaya wameelezea nia yao ya kushiriki katika ujumbe huo, unaoonekana kama nyongeza ya muungano unaoundwa na Marekani baada ya shambulio dhidi ya meli za mafuta zilizokodiawa na Washington na washirika wake nchini Iran .

Hatimaye Uingereza imejiunga na Marekani. Uholanzi itatuma chombo maalumu na helikopta moja kwenda Ghuba kuanzia mwezi Februari. Manuari ya kivita ya Denmark itachukuwa nafasi hiyo katika majira ya Joto, wizara ya jeshi ya Ufaransa imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.