Pata taarifa kuu
IRAN-UKRAINE-AJALI

Ajali ya ndege ya Ukraine: Wataalam wa Ukraine waanza uchunguzi

Ndege ya shirika la ndege la Ukraine International Airlines, ilijaribu kugeuza kuelekea uwanja wa ndege baada ya "tatizo", kulingana na uchunguzi wa awali kutoka Iran.

Nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky ametangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa leo Alhamisi.
Nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky ametangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa leo Alhamisi. REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Boeing 737 ilianguka jijini Tehran Jumatano wiki hii, na kuua watu 176, wengi wao raia wenye uraia pacha wa Iran na Canada.

Nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky ametangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa leo Alhamisi.

"Kipaumbele cha Ukraine ni kujuwa sababu za ajali hii", wakati wataalam 45 wa Ukraine wako Tehran kushiriki uchunguzi.

Sergei Danylov, katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Ukraine, amesema kuwa Kiev inachunguza mambo saba ya ajali hiyo, ikiwa ni pamoja na kufyatuliwa kombora, shambulizi au tatizo la kiufundi.

"Tunachunguza mambo yote hayo, yako saba," Sergei Danylov ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.