Pata taarifa kuu
ISRAEL-IRAN-USALAMA

Benyamin Netanyahu: Israeli 'itajibu' shambulio la Iran ikiwa itashambuliwa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba nchi yake italipiza kisasi kwa yoyote atakayewashambulia, huku akitetea kauli yake ya kuiunga mkono hatua ya Marekani ya kumuua mkuu wa kikosi maalumu cha Iran Jenerali Qassemi Soleimani wiki iliyopita.

Kaimu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Kaimu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. GIL COHEN-MAGEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Yeyote atakayotushambulia atapata majibu mabaya ya kushtukiza," Kaimu Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema, baada ya Iran kurusha makomora kadhaa dhidi ya kambi mbili za jeshi zinazotumiwa na askari wa Marekani nchini Iraq.

Benjamin Netanyahu amesema Israel inaungana na uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa anahitaji kupongezwa kwa kuchukua hatua hiyo kwa utaratibu, ujasiri na umadhubuti.

Iran imebaini kwamba ilifanya mashambulizi hayo kwa kulipiza kisasi kifo cha jenerali Qassem Soleimani, aliyeuawa wiki iliyopita katika shambulio la anga la Marekani nchini Iraq.

Jumapili afisa mwandamizi wa Iran alitishia kuangamiza miji ya Israeli na kuigeuza "vumbi" "ikiwa Marekani itachukua hatua hata ndogo baada ya shambulizi letu la kijeshi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.