Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Arobaini wauawa katika mkanyagano Iran

Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha katika mji wa Kerman nchini Iran, baada ya kukanyangana wakati wa mazishi ya kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Qasem Soleimani, aliyeuawa wiki iliyopita baada ya kushambuliwa na ndege ya kivita ya Marekani nchini Iraq.

watu 35 wameripotiwa kufarika kufuatia kisa cha mkanyagano katika mazishi ya Qasem Soleimani, jenerali wa kikosi maalum cha jeshi la Iran alieuawa na Marekani wiki iliyopita.
watu 35 wameripotiwa kufarika kufuatia kisa cha mkanyagano katika mazishi ya Qasem Soleimani, jenerali wa kikosi maalum cha jeshi la Iran alieuawa na Marekani wiki iliyopita. ATTA KENARE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waombolezaji walikuwa wamekusanyika katika mji huo wa Kerman alikozaliwa Jenerali huyo, kuhudhuria mazishi yake baada ya kifo hicho ambacho kimeleta huzuni mkubwa nchini Iran.

Maafisa wanasema kuwa watu wengine zaidi ya 190 walijeruhiwa katika mkanyagano huo wa watu waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa Jenerali huyo waliyemwita shujaa.

Idadi kubwa ya waombolezaji ilisababisha wengine kukimbilia katika milima ya jirani katika mji huo, ili kufuatilia tukio hilo la mazishi.

Viongozi wa Iran wameendelea kuilaani Marekani na kusema kuwa kumuua kiongozi huyo wa kijeshi, wameipa nguvu ya kuendeleza harakati za kupambana na nchi hiyo.

Mauaji haya yamesabisha uhusiano mbaya kati ya Iran na Marekani, huku wabunge nchini Iran wakipitisha mswada na kuwaita wanajeshi wa Marekani magaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.