Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA-SIASA

Rais wa Lebanon amtaka Hassan Diab kuunda serikali

Rais wa Lebanon Michel Aoun amemteua aliyekuwa Waziri wa Elimu Hassan Diab kuunda serikali mpya. Hii ni baada ya viongozi wa kundi la Hezbolla na washrika wake kumpendekeza baada ya mazungumzo ya saa kadhaa na wabunge.

Hassan Diab mwaka 2012 wakati alipokuwa Waziri wa Elimu Lebanon.
Hassan Diab mwaka 2012 wakati alipokuwa Waziri wa Elimu Lebanon. AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Lebanon Michel Aoun alizindua mazungumzo ya bunge Alhamisi, ambayo yaliahirishwa mara kadhaa, ili kuchagua kiongozi wa serikali atakayechukua nafasi ya Saad Hariri, ambaye alijiuzulu mwishoni mwa mwezi Oktoba kwa shinikizo la waandamanaji. Rais amekua akitaka Hassan Diab ndio aweze kuchukuwa nafasi ya Waziri Mkuu. Hassan Diab alichaguliwa kwa kura 69 na wabunge 39 walijizuia kuchagua mtu yeyote kwenye nafasi hiyo.

Hassan Diab, mhandisi ambaye wananchi wengi wa Lebanon hawamfahamu, aliwahi kuwa Waziri wa Elimu katika serikali iliyotawaliwa na Hezbollah na washirika wake mnamo mwaka 2011. Serikali iliundwa baada ya kuvunjika kwa muungano ambao wakati huo ulikua ukiongozwa na Saad Hariri, ambaye alitangaza Jumatano wiki kuwa hatowania kwenye nafasi ya waziri mkuu, aliokuwa akishikilia kwa miaka kadhaa.

Hassan Diab anakabiliwa na kibarua kigumu, hasa kurejesha usalama na hasaa kuunda serikali ya umoja.

Lebanon imekosa serikali tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, baada ya Waziri Mkuu Saad Hariri kujiuzulu kutokana na maandamano ya wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.