Pata taarifa kuu
LEBAON-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Lebanon: Makabiliano mapya kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama Beirut

Makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yameendelea nchini Lebanon kwa siku kadhaa sasa. Jumapili jioni Desemba 15, makabiliano mapya kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yalizuka karibu na makao makuu ya Bunge jijini Beirut.

Makabiliano katika mji wa Beirut, Desemba 15, 2019.
Makabiliano katika mji wa Beirut, Desemba 15, 2019. ANWAR AMRO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wanaoendelea kupinga utawala waliwarushi maafisa wa polisi mawe na chupa za maji, huku polisi ikijibu kwa gesi ya machozi na kuwasambaratisha kwa maji, kwa mujibu wa mpiga picha wa shirika la habari la AFP.

Watu kadhaa walijeruhiwa katika makabiliano hayo, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Wakibebelea bendera ya Lebanon, waandamanaji, ambao wanaendelea na maandamano yao tangu Oktoba 17 dhidi ya kundi la wanasiasa ambao wanashutumiwa ufisadi, wameandamana Jumapili hii huku wakiimba nyimbo zinazompinga Waziri Mkuu Saad Hariri aliyejiuzulu.

Wakati huo huo waandamanaji wenye hasira Kaskazini mwa Lebanon, wamezichoma moto ofisi za vyama viwili vikuu vya kisiasa, shirika la habari linalomilikiwa na serikali limesema.

Katika wilaya ya Akkar kaskazini mwa nchi hiyo, washambuliaji walivunja madirisha na kuteketeza moto ofisi ya chama cha waziri mkuu aliyejiuzulu Saad Hariri katika mji wa Kharibet al-Jindi. Katika mkasa mwingine, washambuliaji walivamia ofisi ya chama kikubwa zaidi bungeni kinachoongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje Gebran Bassil na kinachoshirikiana na Rais Michel Aoun. Chama hicho pia kimesema vitu katika ofisi yao iliyoko mji wa Jedidat al-Juma pia vimechomwa moto na kuharibiwa.

Lebanon inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi kiuchumi kuwahi shuhudiwa kwa miongo mingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.