Pata taarifa kuu
ISRAELI-UCHAGUZI-SIASA

Israel: Benny Gantz ashindwa kuunda serikali

Mpinzani wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Benny Gantz amemwambia rais wa Israeli kwamba ameshindwa kuunda serikali ya umoja. Hivyo Israeli inajiandalia uchaguzi mpya wa wabunge.

Benny Gantz katika mkutano na waandishi wa habari huko Tel Aviv baada ya kushindwa kuunda serikali, Novemba 20, 2019.
Benny Gantz katika mkutano na waandishi wa habari huko Tel Aviv baada ya kushindwa kuunda serikali, Novemba 20, 2019. REUTERS/Amir Cohen
Matangazo ya kibiashara

Benny Gantz amesema amejitahidi kufanya "anacho kiwezo" kujaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa, bila mafanikio.

Wakati sheria ilimpa hadi Jumatano saa 5:59 usiku kuwa ameunda serikali ya umoja, lakini ameamua kuachia ngazi na kutangaza kwamba ameshindwa. "Kiongozi wa chama cheupe na Bluu, Benny Gantz amezungumza na Rais Reuven Rivlin ili kumwambia kuwa ameshindwa kuunda serikali," chama chake cha kisiasa kimesema.

Benyamin Netanyahu, waziri mkuu anayemaliza muda wake na mpinzani wake Benny Gantz hawakupata viti vingi bungeni vinavyo muwezesha mmoja kati ya wawili hao kuunda serikali.

Awali Rais Reuven Rivlin alimwagiza Benjamin Netanyahu, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, kuunda serikali. Lakini Netanyahu, anayeongoza kambi ya mrengo wa kulia na wa kidini ambayo ina wabunge 54, alishindwa kupata kura za kutosha kufikia viti 61.

Rais alimgeukia Benny Gantz na kumuagiza kuunda serikali, ili kuzuia uchaguzi wa tatu chini ya mwaka mmoja.

Hata hivyo Benny Gantz ameshindwa kumshawishi Avigdor Lieberman - kiongozi wa chama kisicho na msimamo cha Israel Beitenou.

Moja ya matumaini ya Gantz ilikuwa kupata uungwaji mkono wa chama cha Avigdor Lieberman ili kuweza kuunda serikali ya mungano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.