Pata taarifa kuu
ISRAELI-UCHAGUZI-SIASA

Israel: Lieberman akataa kumuunga mkono Netanyahu au Gantz kama waziri mkuu

Avigdor Lieberman, kiongozi wa chama kisicho na msimamo ambacho uungwaji wake mkono unaweza kuwa muhimu kwa muungano nchini Israeli, amesema kuwa hamuungi mkono Benjamin Netanyahu au mpinzani wake Benny Gantz kwa uundwaji wa serikali ya muungano.

Naftali Bennett, Waziri mpya wa Ulinzi (sehemu ya mbele ya picha) katika mkutano wa baraza la mawaziri nchini Israeli, Novemba 17, 2019.
Naftali Bennett, Waziri mpya wa Ulinzi (sehemu ya mbele ya picha) katika mkutano wa baraza la mawaziri nchini Israeli, Novemba 17, 2019. Gali Tibbon/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Katika hali ya sasa tuko njiani kuelekea uchaguzi mpya," Lieberman, kiongozi wa chama cha Israell Beiteinou, aamese akatika mkutano na waandishi wa habari Jumatano wiki hii jijini Jerusalemu, wakati Benny Gantz anasalia na saa chache ili kuweza kuunda serikali.

Benjamin Netanyahu na Benny Gantz walishindwa kueneza viti vya wabunge vinavyohitajika ili kuuunda serikali katika uchaguzi wa wabunge wa mwezi Septemba. Wawili hao pamoja na washirika wao walishindwa kupata kupata kura zinazohitajika ili kuwa na wingi wa viti bungeni.

Awali Rais Reuven Rivlin alimwagiza Benjamin Netanyahu, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, kuunda serikali. Lakini Netanyahu, anayeongoza kambi ya mrengo wa kulia na wa kidini ambayo ina wabunge 54, alishindwa kupata kura za kutosha kufikia viti 61.

Rais alimgeukia Benny Gantz na kumuagiza kuunda serikali, ili kuzuia uchaguzi wa tatu chini ya mwaka mmoja.

Benny Gantz ana hadi saa 5:59 usiku kuwa ameunda serikali ya muungano.

Moja ya matumaini ya Gantz ilikuwa kupata uungwaji mkono wa chama cha Avigdor Lieberman ili kuweza kuunda serikali ya mungano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.