Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-USALAMA

Afghanistan: Watu saba wauawa katika shambulio la bomu

Takribani watu saba wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari, ambao ulitokea saa 7:25 asubuhi katika eneo la PD15, kaskazini mwa mji mkuu, karibu na makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani.

Mashambulizi ya kujitoa mhanga yameendelea kusababisha vofo vingi na kuharibu mali Afghanistan.
Mashambulizi ya kujitoa mhanga yameendelea kusababisha vofo vingi na kuharibu mali Afghanistan. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Nasrat Rahimi.

Chanzo kingine katika wizara hiyo kimesema shambulio hilo limekuwa limelenga msafara wa magari ya serikali kwenye barabara kuu. Hata hivyo hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.

Afghanistan imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya hapa na pale, mashambulizi ambayo yanadaiwa kutekelezwa na makundi mbalimbali yenye silaha, hasa kundi la Taliban.

Mashambulizi hayo yamesababisha watu wengi kupoteza maisha na mamia kupoteza baadhi ya viungo vyao vya mwili, kama mikono na miguu.

Umoja wa Mataifa umeendelea kulaani mashambulizi hayo yanayowalenga raia na kusababisha nchi hiyo kuendelea kukosa utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.