Pata taarifa kuu
IRAQ-MAANDAMANO-USALAMA

Mgomo waendelea kuathiri uchumi wa Iraq

Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Iraq na Kusini mwa nchi hiyo wamefunga barabara na ofisi za Serikali katika kile ambacho kinaelezwa ni mfululizo wa mgomo wa kutotii Serikali wakishinikiza mabadiliko ya mfumo mzima wa kisiasa.

Waandamanaji wakishiriki katika maandamano dhidi ya ufisadi, ukosefu wa ajira na huduma duni, Baghdad, Iraq, Oktoba 27, 2019.
Waandamanaji wakishiriki katika maandamano dhidi ya ufisadi, ukosefu wa ajira na huduma duni, Baghdad, Iraq, Oktoba 27, 2019. REUTERS/Thaier Al-Sudani
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yalianza Oktoba Mosi mwaka huu ambapo wananchi walikuwa wanapinga kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ukosefu wa ajira nchini Iraq.

Hata hivyo waandamanaji walikabiliwa na nguvu kubwa ya Serikali ambapo ilitumia jeshi na polisi kujaribu kuzima maandamano ambayo yalikuwa yameanza kuenea nchi nzima.

Maandamano hayo sasa yamepata uungwaji mkono kutoka kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, vyuo vikuu na mashirikisho ya vyama vya wafanyakazi ambao nao wameamua kuingia barabarani kushinikiza Serikali kujiuzulu.

Viongozi wa maandamano haya wameapa kuendelea kufunga ofisi za Serikali na barabara hadi pale wale iliyowaita wala rushwa watakapoondoka mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.