Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-MAREKANi-USHIRIKIANO-USALAMA

Syria: Trump aonya Uturuki, baada ya kupata shinikizo

Uamuzi uliotangazwa na Donald Trump wa kuwaondoa askari wa Marekani waliotumwa nchini Syria kutoka kwenye mpaka wa Kaskazini na kuachia nafasi jeshi la Uturuki umekosolewa ndani na nje ya Marekani na hususan katika chama cha Republican.

Donald Trump katika Ikulu ya White House, Oktoba 7, 2019.
Donald Trump katika Ikulu ya White House, Oktoba 7, 2019. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya viongozi vigogo serikalini kutokachama cha Republican serikalini wamekosoa uamuzi huo, huku wakitilia mashaka hatua ya jeshi ya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi ambao ni washirika wa Marekani katika vita dhidi ya kundi la Islamic State.

Vigogo hao kutoka chama cha Republican wanabaini kwamba ikiwa askari wa Marekani wataondoka kwenye mpaka na Uturuki na kuachia jeshi la Uturuki kuendesha operesheni katika eneo hilo la mpakani, kuna hatari jeshi hilo kushambulia waiganaji wa Kikurdi wanashirikiana na Marekani katika vita dhidi ya Islamic State.

Serikali ya Marekani inaendelea kutoa taarifa ya kurekebisha msimamo wake wa wawali ambao unaendelea kukosolewa na wengi nchini Marekani.

Wakati huo huo Seneta wa Marekani Lindsey Graham na mshirika wa karibu wa Rais Donald Trump amesema huenda akaiitisha bunge la Congress ili libatilishe uamuzi wa Rais wa Marekani wa kuondoa vikosi vya Marekani kutoka katika mpaka wa Syria na Uturuki.

Lindsey Graham ambaye ni mwenyekiti wa kamati sheria katika bunge la Congress ameuelezea uamuzi wa Rais Trump wa kuondoa wanajeshi wake katika mpaka huo kama janga kwa Marekani, raia wa Syria na washirika wake wapiganaji wa Kikurdi.

Lindsey Graham ameongeza kusema kuwa hatua ya kuondoa wanajeshi wa Marekani ni kuwatenga wapiganaji wa Kikurdi ambao walikua washirika wakubwa wa Marekani katika harakati za kulisambaratisha kundi la wapiganaji wa kijihadi, Islamic State.

Kwa upande wake Serikali ya Uturuki kupitia kwa Rais Recep Tayyip Erdogan imesema itaanzisha operesheni ya kujilinda dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kama walivyokubaliana na Rais Trump kwa njia ya simu huku wakidai kuwa wapiganaji wa kikurdi ni magaidi.

Umoja wa Ulaya umeonya kuwa hatua zinazotaka kuchukuliwa na Uturuki za kukabiliana na Wakurdi zitahatarisha usalama wa raia nchini Syria na Uturuki yenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.