Kiongozi wa kiroho wa Kishia aunga mkono madai ya waandamanaji Iraq
Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha nchini Iraq baada ya kuzuka kwa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji katika maeneo mbalimbali katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.
Imechapishwa:
Maandamano haya yameendelea licha ya serikali, kutangaza hali ya kutotembea usiku katika mji mkuu Bangdad.
Waandamanaji wanasema wanataka serikali iboreshe huduma mbalimbali kama ukosefu wa mara kwa mara wa umeme na maji.
Makabiliano hayo yamesabisha waandamanaji wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, baada ya kushambuliwa na risasi za moto, na wengine kulazimishwa kukimbia wakihofia usalama wao.
Umoja wa Mataifa umelaani polisi kutumia nguvu katika maandamano hayo, huku kiongozi wa kiroho wa Kishia Grand Ayatollah Ali Sistan akiitaka serikali kusikiliza madai ya wanadamanaji.