Pata taarifa kuu

Israel: Benjamin Netanyahu afuta ziara yake New York

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliorudiwa mapema wii hii nchini Israel yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu anaye maliza muda wake Benajamin Netanyahu hakupata wingi wa viti katika Bunge.

Ingawa  hakupata wingi wa viti bungeni, Benjamin Netanyahu ana imani ya kuunda serikali mpya.
Ingawa hakupata wingi wa viti bungeni, Benjamin Netanyahu ana imani ya kuunda serikali mpya. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Vyama viwili vikuu, Likud cha Netanyahu na kile cha samawati na nyeupe cha Bw Gantz, vimekabana koo huku waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu akikabiliwa na kazi ngumu ya kuendelea kushikilia nafasi yake.

Kwa sasa mazungumzo kati ya vyama ili kuunda serikali ya umoja yanaelezwa kuwa ni magumu. Kutokana na hali hiyo ya mvutano na kushindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi wa wabunge, Waziri Mkuu anaye maliza muda wake Benjamin Netanyahu amefuta ziara yake mjini New York kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki ijayo.

Benjamin Netanyahu anathamini mikutano mikubwa ya kimataifa inayomruhusu kukutana na viongozi kutoka ulimwenguni kote. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York ni moja ya mikutano hiyo anayothamini bw Netanyahu.

Lakini kwa upande wa Lahav Harkov, mwandishi wa masuala ya siasa wa gazeti la kila siku la Jerusalem Post, amesema matokeo ya kukaribiana kwa kura katika uchaguzi wa wabunge yalmemlazimisha Benjamin Netanyahu kufuta ziara hii ya mwaka huu. "Nadhani hali ya Netanyahu ikoi hatarini kwa sasa ambapo anahitaji kuona ikiwa ataendelea kuwa Waziri Mkuu au la," Lahav Harkov ameongeza. Ikiwa atapewa nafasi ya vyama atakavyoungana navy, atapewa muda usiozidi ili awe ameunda muungano huo. Na hivyo kila siku, kila saa inahesabiwa.

"Jambo la wakati ambalo ni muhimu. Lakini labda lina manufaa madogoni mkutano wake na Donald Trump uliopangwa hivi karibuni, Dan Shapiro amesema.

Dan Shapiro alikuwa balozi wa Marekani nchini Israeli wakati wa utawala wa Obama. "Ikiwa anaona inaweza kumsaidia kuwaambia washirika wake watarajiwa wa muungano na wananchi wa Israeli kwamba anahitaji kutafuta njia itakayomuwezesha kusalia kwenye nafasi yake, nadhani angefanya hivyo kufanya ziara hiyo. Na inaweza kuwa ishara kuwa Trump ameanza kuchukua hatua za kujitenga na Netanyahu.

Siku ya Jumatano usiku, rais wa Marekani pia alisisitiza kwamba uhusiano wa utawala wake "uko pamoja na Israeli", kauli inayo ashiria kwamba anaweza kushirikiana na Waziri Mkuu mwingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.