rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Saudi Arabia Iran Marekani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulizi dhidi ya mafuta ya Saudi Arabia: Donald Trump aionyooshea kidole Iran

media
Miundo mbinu ya kuzalisha mafuta ya kampuni ya Aramco, Abqaiq, mashariki mwa Saudi Arabia, Septemba 14, 2019. REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump ameilamu Iran kwa kushambulia miundo mbinu ya kuzalisha mafuta ya Saudi Arabia iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo muhimu kupanda.


Hata hivyo, Iran imekanusha madai hayo na kusema hayana ukweli wowote.

Trump amesema yuko tayari kuisaidia Saudi Arabia kukabiliana na hali hii licha ya kutotaka kuingia kwenye vita na nchi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, anatarajiwa kwenda jijini Riyadh hivi karibuni kujadili hatua ya kuchukua, wakati huu uchunguzi ukiendelea kubaini iwapo kweli Iran ilihusika na mashambulio hayo.

Marekani ilitoa picha za setilaiti na kunukuu taarifa za ujasusi kuthibitisha madai yake kwamba Iran ilikuwa nyuma ya mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta vya Saudia.

Katika ujumbe wake alioandika kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumapili, Rais Donald Trump hakuishutumu moja kw amoja Iran, lakini alisema kuwa hatua za kijeshi zinaweza kuchukuliwa pale muhusika wa mashambulio atakapojulikana.