Pata taarifa kuu
ISRAELI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Wabunge wawili kutoka chama cha cha Democrat Marekani wapigwa marufuku kuingia Israeli

Israeli imepiga marufu wabunge wawili wa chama cha cha Democrat nchini Marekani Rashida Tlaib na Ilhan Omar kuingia nchini humo. Wabunge hao walikuwa wamepangilia kuzuru Palestina.

Rais wa Marekani, Donald Trump, Wabunge wa Marekani Ilhan Omar, Rashida Tlaib na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kwenye picha ya kumbukumbu.
Rais wa Marekani, Donald Trump, Wabunge wa Marekani Ilhan Omar, Rashida Tlaib na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kwenye picha ya kumbukumbu. REUTERS/File Photos
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo uliotangazwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Tzipi Hotovely, unakuja kufuatia kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Uamuzi huo wa Israeli umesababishwa na wito kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump na unaweza kuwa na athari kwa uhusiano kati ya Israeli na Chama cha Democrat nchini Maekani.

Wizara ya Mambo ya ndani ya Israeli ndio ilitangaza rasmi kuwa wabunge hao wawili kutoka Marekani hawataweza kuingia Israeli. Uamuzi ambao unafuatia siku kadhaa za mjadala kwenye ziara hii ya wawakilishi hao wawili wa Baraza la Wawakilishi Ilhan Omar na Rashida Tlaib, mwandishi wetu Jerusalem, Michel Paul, amekumbusha.

Israel imeamua kuwawekea vikwazo vya usafiri wabunge wawili wa chama cha Democratic nchini Marekani baada ya Rais Trump kuiomba nchi hiyo kuwapiga marufuku.

"Itaonesha udhaifu mkubwa" ikiwa Israel itawaruhusu Ilhan Omar na Rashida Tlaib kuzuru taifa hilo, " Donald Trump alisema.

Wawakilishi hao wa Democrat ni wakosoaji wakubwa wa utawala wa Rais Trump na wa Israel, huku wakiunga mkono kususiwa kwa Israel kutokana na mateso yake dhidi ya Wapalestina. Uamuzi wa kuwanyima wabunge hao wa kike kibali cha kuingia Israel huenda ukazidisha ukosoaji wa Democrat dhidi ya Israel kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani hapo mwakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.