Pata taarifa kuu
PALESTINA-UN-JAMII

UNRWA yaahidiwa dola milioni 110

Shirika la misaada la umoja wa mataifa kwa wakimbizi wa Palestina (UNRWA), linaendelea kukusanya fedha licha ya dola milioni 110 ambazo limeahidiwa.

Wakaazi wa mji wa Gaza wakipewa chakula katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Mei 9, 2019.
Wakaazi wa mji wa Gaza wakipewa chakula katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Mei 9, 2019. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Wafadhili wameahidi kuchangia kiasi cha dola milioni 110 katika Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA), na kuliwezesha shirika hilo kuenedelea na kazi yake katika Ukingo wa Magharibi na maeneo mengine ya Palestina.

Hata hivyo Kamishna Mkuu Pierre Krahenbuhl amesema akiwa mjini New York, kwamba fedha hizo hazitotatua changamoto wanayoikabili lakini zitasaidia kuendeleza huduma za UNRWA kwa miezi kadhaa.

"Hafla nyingine ya kukusanya fedha kutoka kwa wafadhili itafanyika pembezoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Septemba", ameongeza Pierre Krahenbuhl .

Mwaka jana, Marekani iliamua kusitisha kufadhili mipango yake iliyokuwa ikiwasaidia Wapalestina milioni 5, na hivyo kuingiza katika hali ngumu ya kifedha shirika la UNRWA.

Wakati huo huo mkwe wa rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha mpango wake wa kiuchumi unaokusudia kuwaletea mafanikio raia wa Palestina. Mpango huo wa Kiuchumi wa Mashariki ya Kati, uliopewa jina la "Amani hadi Mafanikio" umewasilishwa na Jared Kushner katika mkutano wa siku mbili ulioanza jana, kuhusu maendeleo ya kiuchumi ya Wapalestina unaofanyika mjini Manama, Bahrain.

Hata hivyo Chama cha Ukombozi wa Wapalestina (PLO) kimeuelezea mpango huo kuwa ni wenye ahadi zisizokuwa na uhalisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.